MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

Sunday, January 20, 2013

Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kufanya Maamuzi Sahihi Katika Maisha

   Katika Maisha yetu ya kila siku mara nyingi tunajikuta katika mazingira yanayotulazimu kufanya maamuzi magumu au kuchagua kitu katikati ya vitu vingi ambavyo vinatuchanganya akili.  Wengi wetu kwa ugumu huu wamejikuta wakifanya maamuzi mabovu na kuchagua chaguzi mbovu ambazo ama ziliwapa hasara  au ziliharibu kabisa muelekeo au mustakabali wa maisha yao.  Ndio maana wenzetu wa magharibi (Ulaya) wanamsemo usemao “Life is how you make Decisions” Maisha ni vile unavyofanya maamuzi.

ITAMBUE HAIBA YAKO (Know your Personality)

Jitambue Ya Chris Mauki.......ITAMBUE HAIBA YAKO (Know your Personality)


  Katika utafiti wakuchunguza athari za msongo wa mawazo katika moyo, madaktari Mayer friedman na Ray Roseman waliweza kuwaweka watu katika makundi ya haiba mbili; yaani haiba kundi A and haiba kundi B.
 
Madaktari hawa waligundua kuwa hata kama kazi na aina ya maisha ingefanana, watu wa haiba kundi A wangekuwa na nafasi mara 3 kuteseka na msongo wa mawazo, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu n.k. na watu hawa mara nyingi huwa wanamaudhi kwa jinsi wanavyojibu au kuongea na wengine, na hili limekuwa likiwaongezea msongo wa mawazo maradufu.

Makundi haya yamewekwa ili kukuwezesha wewe kujua uko upande gani. Usichanganyikiwe wala kushtuka pale utakapojikuta una tabia za makundi yote mawili, mara nyingine inaamaanisha kuwa uko vizuri katika kuhakikisha mambo yanafanyika inavyotakiwa au unavyotaka yawe. Ila kama unajikuta unatabia zaidi ya nusu za haiba kundi A inabidi uchukue uamuzi wa kutafuta kubadilika au kubalisha mtazamo ulionao katika maisha, kabla haujajihatarishia maisha yako wewe mwenyewe.

Haiba Aina ‘A’
-       Ni watu wa ushindani katika kila kitu wafanyacho.
-       Watu wenye haiba ya kutumia nguvu na kulazimishisha
-       Hufanya mambo yao mengi kwa haraka
-       Huwa na uchu wa kupandishwa vyeo na kujulikana katika jamii. (Hatakama hawana sifa).
-       Hutaka sana kujulikana na kuheshimiwa kwa kile walichokifanya.
-       Hukasirishwa kwa haraka na watu au matukio fulani
-       Huongea mara kwa mara kwa kufoka au kwa vitisho
-       Hupenda kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
-       Hutembea na hata kula kwa haraka
-       Mara nyingi kuchukizwa sana pale wanapocheleweshwa 
-       Hujali sana muda na kukazana kumaliza mambo kwa muda ulipangwa (meating deadlines)
-       Kila mahali huwepo kwa wakati na kwa muda muafaka.
-       Mara kwa mara misuli yao ya uso huonyesha, kumaanisha, kuogopesha au ukali,
Haiba Aina ‘B’
-       Sio watu wa ushindani  mfano, makazini, michezoni, masomoni n.k.
-       Ni watu walio rahisi, na huyakubali mazingira, hufanya vitu taratibu na kwa kufuata kanuni.
-       Huendelea na kuchukuliana na hali ya kazi iliyopo.
-       Huridhika na nafasi walinayo katika kijamii.
-       Hawahitaji kujulikana  au kutambulika katika jamii au hata katika matukio.
-       Sio rahisi sana kuwaudhi.
-       Mara nyingi hufurahia sana wanapokuwa pekeyao.
-       Ni wavumilivu.
-       Hupendelea kufanyakitu kimoja kwa muda muafaka kabla ya kwenda kwenye kitu kingine.
-       Hutembea, na kula kwa nafasi na utulivu.
-       Hawakimbizwi sana na muda, sio wakukimbizana sana na kumaliza kazi.
-       Mara nyingi ni wachelewaji.
-       Nyuso zao ni za kufurahi na sio za mikunjo.

KWANINI UKO VILE ULIVYO?
Vyovyote haiba yako ilivyo na kwa vyovyote unavyowachukulia wenye wale tabia ngumu fahamu kuwa mfano huo ulishakuwepo miaka mingi iliyopita, labda zaidi ukiwa mtoto ndio ilikuwa chanzo cha vile ulivyo leo; Mwanasaikolojia mmoja aliuita mfumo huu..“A child is a father of a man” yaani
Mambo tunayoyaona au unayoyaona kwa mtoto hutupa picha halisi ya ukumbwa wake utakavyokuwa. Zaidi ya asilimia sitini ya yote yanayoendelea maishani mwetu leo yanachangiwa na makuzi yetu tukiwa watoto
Wengi wetu tumejiharibia misingi yetu ya uwezo wa kuishi na watu wenye tabia ngumu na hivyo kujikuta tunaumizwa tokea tukiwa watoto wadodo. Habari njema ni kwamba hakuna ulazima wa kubaki vile ulivyo, mabadilko yanawezakana, inawekana katika hatua yoyote kubadili mtazamo au muonekano wako na kuboresha ujasiri wako.
Tujaribu kuangalia baadhi ya sababu zinazosababisha mtu kujiona au kujitazama vibaya, hii itakuwezesha wewe kujua uko wapi na kwanini.
  1. Watu wa kwanza kabisa waliowahi kuwa karibu na wewe ni baba na mama yako au yoyote aliyechukua nafasi yao, mfano mlezi, babu, bibi nk. Kutokana na mtazamo wao juu yako, hapo wewe umetengeneza au kuzalisha mtazamo juu yako mwenywe najinsi unavyojithamini au kutojithamini. Kwa lugha rahisi ni kwamba, jinsi unavyojiangalia ulivyo leo kunatokana kwa kiasi kikubwa na jinsi wao walivyokuwa wanakutazama, kama walikuona wewe lofa na mjinga basi kuna uwezekano mkubwa na wewe leo utajiona lofa tu.

Najua wapo wazazi wasio na hekima wala wema kwa watoto wao, huwasababishia watoto wao majeraha ya kimwili, kihisia na hata kiakili, uzuri ni kwamba fungu la wazazi hawa ni dogo. Ingawa inawezekana sana kwa wazazi au walezi au watu wazima wowote kusababisha majeraha na athari kwa watoto mara nyingine pasipo kujua kwamba wanafanya hivyo. Katika kuongea na wazazi lukuki nimegundua kwamba asilimia kubwa ya watoto wameharibiwa na wazazi wao wenyewe, pasipo wazazi hawa kujua kuwa wanawaharibu watoto wao.

  1. Wazazi ambao huwalinda na kuwatetea sana watoto wao, wakijaribu kuwafanyia kila kitu kwa niaba ya watoto hao, kwa njia hii wazazi hawa hutengeneza watu wazima (wababa au wamama) wenye utegemezi mkubwa, wasioweza kufanya kitu chochote wenyewe wala kusimama kwa miguu yao wenyewe. Unakuta hata kazi za shuleni mama ndiyo anafanya, mtoto anakuwa hata kuosha mwili wake hajui, na hawa ndio wale ambao ndoa huwashinda mapemaaa.

  1. Wale wazazi au walezi ambao hutoa mahitaji kwa watoto wao lakini hushindwa kuonyesha kwa matendo upendo wao kwa watoto wao (mfano. Kuongea nao, kucheka nao, kucheza nao n.k.) hutengeneza kizazi kinachoamini kuwa hakipendeki, hakina mvuto, kisicho na thamani na kisichostahili kupendwa. Baba haijalishi unatoa mahitaji yote yanayohitajika nyumbani kwako, hilo sio pekee watoto wako wanalolihitaji kutoka kwako, wape muda wakuwa pamoja nao, waruhuru kucheza na wewe kidogo, toka pamoja nao, jibu baadhi ya maswali yao, waruhusu kujuwa kumbe baba au mama anaweza kuwakaribu na sisi pia.


  1. Wazazi au walezi ambao kila mara humwekea mazingia mtoto kujiona aliyeshindwa, kila wakati ni wakufeli tu, wazazi hawa ni wale wanaosema kwa nini mtoto asijitahidi, kwanini asiwe wa kwanza darasani, ni mpumbavu n.k.. hali hii huharibu kabisa imani ya mtoto kwake yeye mwenyewe, huua kule kujiamini kwake na pia kutokiamini kile anachokifanya.
Yawezekana kuna vitu vilivyoonekana katika makuzi ya mtoto ambavyo hakuna wa kulaumiwa lakini bado vitu hivi huathiri sana kujiamini na kujithamini kwa mtoto yule.
Mtoto au watoto wanaohama hama au kuhamishwa shule mara kwa mara, kwa sababu zao binafsi au kwa sababu ya kuhama hama kwa wazazi hupata shida yakujiona wapweke kwa maana kila wakati hupata kazi ya kutengeneza marafiki wapya na kwamuda fulani hali hii huathiri haiba zao na kujenga kitu tunachokiita “inferiority complex”

Tufanye nini??
Kitu cha kwanza ni kukubaliana na ukweli kwamba mtazamo wako (jinsi unavyojitazama) hubadilika badilika. Tena hubadilika kiasi ambacho mara nyingine huwezi kutambua. Unaweza kuchagua mwenyewe jinsi unavyotaka mtazamo wako uwe. Kwa mfano;
  1. Kufanikiwa au kushindwa
Jaribu kutoangalia nyuma kule ulikowahi kushindwa zaidi, kila mtu anahistoria ya kushindwa sio wewe tu. Wacheza mpira maarufu duniani, mara nyingine hukosa magoli rahisi kabisa lakini hakuna hata mmoja aliye acha kucheza au kuharibu fani yake kwa sababu ya kukosa goli. Wala hakuna aliyekiri kuwa yeye sio bora kwa sababu tu ya kukosa goli moja. Ni vema kukumbuka kule tulikowahi kushindwa kama tu tunataka kujifunza katika makosa yetu, na sio kwa kutaka  kujisononesha na kujilaumu kwa namna tulivyokosea. Jifunze kuziacha historia za kufeli na kushindwa zifukiwe katika yaliyopita.

Tengeneza mafanikio yako wewe mwenyewe anza katika hali ya chini kabisa, chagua vile vitu usivyo viweza kabisa kuvifanya mfano; Kuzungumza mbele ya watu, kuimba, kuogelea, kuwa kwenye usaili, kusimama mbele ya kamera n.k anza kuvifanya kwanza kupitia ufahamu wako (viwaze akilini) hali hii inaitwa (creative visualization) ni njia majawapo bora ya kufanya mazoezi ya vile tunavyoshindwa katika fikra zetu, kwanza jitahidi kujitazama fikrani ukiwa au ukifanya vitu hivyo kwa ushindi hadi ufahamu wako utakapoizoea hali hiyo na kuacha kutuma jumbe za kushtuka (kupanick) au uwoga wakati utakapokuwa unafanya vitu vile kihalisi.

Katika kufanya mazoezi ya kufikiria kimtazamo, chagua kufanya katika utulivu mchana au jioni. Muda kabla hujaenda kulala ni mzuri zaidi. Rudia zoezi hili mara kwa mara mpaka uzoee na fikra zizoee.

  1. Andika vile vitu uvipendavyo juu yako mwenyewe, kama kuna mtu anayesema kuwa hana kitu cha kuandika basi mtuhuyo hajafikiri kwa undani au ni mwongo, kila mtu anakitu chema ndani yake.
Kama ukishaandika vitu hivi, angalia tabia ya vile vitu ulivyoviandika pale, kama vitu hivyo vikifanywa na mtu baki usiyemjua je utasema yeye ni mtu mbaya? Kama sio, kwa nini wewe unajiona usiyefaa na uliyejaa mabaya tu?
Badala ya kutazama yale yaliyo mabaya na yakushindwa katika historia yako tazama mafanikio yako. Kila mmoja ana mafanikio ya aina fulani, hata kama ni madodo kiasi gani. Hata kama unatazama yale yaliyowahi kufanyika huko awali basi yatazame katika mtazamo chanya. 

Wengi wetu hatuchukui muda kujiuliza vyanzo vya mitazamo yetu hasi, tunaamua kuikubali tu na kuikumbatia na kuifanya asili yetu. Ila mara tu utakapo gundua kuwa tatizo sio lako wewe bali ni mazingira uliyokuziwa au aina ya wazazi uliokuwa nao basi utaacha kujidharau.
Wako watoto wanaofurahia kupelekwa shule za bweni mbali na nyumbani, ila wako ambao hawapendi kabisa lakini wanalazimishwa, hali hii hupandikiza ndani ya watoto hawa upweke, hofu, msongo wa mawazo na kutokutulia (nazungumzia utulivu wa ndani) jambo ambalo huendelea hata katika utu uzima wao. Wako wengi ambao tabia zao za leo zilianza kuharibikia katika shule za bweni mbali na wazazi kwa mfano tabia za kusagana au kuingiliana kinyume na maumbile.

Sisi tumeumbwa katika mifumo na vipindi mbalimbali, mara nyingine tuko chanya (watu wema, wazuri) na mara nyingine tunakuwa hasi (watu wabaya). Kama mtoto atakuwa akiambiwa kila wakati kuwa “kamwe huwezi kuwa na akili kama dada yako” maneno haya hufanyika halisi kwake. Je hujawahi kusikia mtu akisema “mimi sijui kuogelea”, “mimi sijui kama nitaolewa” “Kamwe sitokaa niendeshe gari” , “Mimi sitokaa nijue kiingereza”, “Mimi na kuimba ni tofauti” Haimaanishi kama watu hawa wangeanza kujifunza au kuzaliwa katika mazingira ya vitu hivi, wangevishindwa. Labda kuna sehemu mtu au watu fulani waliwasemea kutoweza au kushindwa na huo ukawa mwanzo wa kuwekewa kizingiti cha ujuzi ndani yao.

Wakati wowote mtu anapojisemea jambo, au neno lililo baya, lisilojenga, lakushindwa, kama utalisema kwa sauti au utalifikiria akilini, katika hali yoyote ile jambo hili hulazimisha uhalisi wa maneno yale kuingia katika mfumo wa maisha yako na kutenda kazi kwa hiyo jifunze kukataa, kukanusha na jitahidi kutenda kinyume na zile sentensi mbaya juu yako. Kama tunaamini utendaji wa kazi wa yale tunayojisemea au kusemewa vibaya basi hata yale tunavyojisemea au kusemewa vema hutenda kazi pia. “If negative proclamation works, surely positive proclamation must work too” Amua kubadilisha yale unayojisema au yale unayosemewa. Badili yale yaliyo negative (yakufeli) yawe positive (yakuweza). Kama hujiamini wewe mwenyewe wala hujithamini, basi utakubali kirahisi kila neno gumu na baya utakaloambiwa na kila mwenye tabia ngumu na kama utayakubali unayoambiwa au unayorushiwa hutaweza kamwe kukabiliana na ushindani kutoka kwa mtu au watu wenye tabia ngumu. Kumbuka daima udhaifu huanzia kwako mwenyewe.

Ukishajifunza kupunguza kujilaumu na kujipinga mwenyewe na kuboresha jinsi unavyojitazama basi utakuwa salama katika kukabiliana na maneno na matendo magumu toka kwa yeyote mwenye tabia ngumu. Na kwa kuwa umejifunza vizuri kujielewa basi sasa waweza kuwaelewa vizuri zaidi wale wenye tabia ngumu. Sasa utaweza kuelewa kuwa kuna kitu kimemfanya au kimewafanya wawe vile walivyo. Mara utakapoweza kumwonea huruma yeyote, haijalishi anatisha kiasi gani basi hawezi tena kukuathiri kwa vyovyote vile.

Kwa jinsi ujasiri wako unavyoongezeka, unaweza pia kuziweka katika matendo mbinu nyingine nyingi za kushuhulika na watu wenye tabia ngumu. Utajikuta unaweza kukabiliana nao na pia kuchukuliana nao katika mazingira tofauti na pia hata katika nyakati ambazo hutakuwa unafanya vizuri katika jambo fulani, hautajilaumu na kujishusha, bali utajisifu kwa kukazana na kujitahidi hata kama haukubahatika.


Chris Mauki
Social and counselling psychologist
PhD candidate
University of Pretoria
chriss@udsm.ac.tz

Jitambue Ya Chris Mauki.....JIFUNZE NAMNA YA KUJISAIDIA MWENYEWE (Self Help Skills)

Utafiti uliofanywa katika maeneo mengi katika nchi zilizo endelea na zinazoendelea unaonyesha kuwa watu wengi bado wanahitaji kiwango kikubwa cha uwezo wa kujisaidia wenyewe.  Hata katika nchi kama marekani ambayo teknolojia ni kubwa lakini watu pia wanakiu kubwa ya jinsi ya kujua kujisaidia wenyewe katika baadhi ya mambo yanayowasibu kimwili, kihisia na maisha kwa ujumla

Wachunguzi wakubwa wa maswala ya kisaikolijia Richard na Tony Robbins wanaafiki kwamba yawezekana kabisa tukarekebisha na kuweka sawa vile visivyokaa sawa katika miili yetu au akili zetu pasipo kutegemea msaada wa daktari au mshauri.

Watu wengi ulimwenguni wanapata msada wa ujuzi huu kupitia kuenea kwa mtandao wa intanet na vitabu vya ujuzi huu vilivyo vingi sana (self help books).
Takwimu zinaonyesha wamarekani walitumia zaidi ya dola 563 milioni kwa manunuzi ya vitabu vya ujuzi wa kujisaidia mwenyewe, na pia zaidi ya tovuti 12000 za masuala ya afya ya akili “mental health” hutumika nchini marekani.  Yote hii ni watu kutafuta uwezo wa kujisaidia zaidi ya kutegemea kusaidiwa  hasa katika mambo ya afya ya akili, hisia ,nk. Zaidi ya 40% ya tovuti za masuala ya afya kutumiwa na watu hasa katika kutafuta kufahamu juu ya tatizo la kupoaaza moyo na upweke (depression).

Huu ni wakati wa kila mmoja kujua jinsi ya kurekebisha maumivu yake na kuponya majeraha yake mwenyewe. Hii  inawezekana.

Habari au taarifa nyingi za namna ya kujisaidia binafsi zimekuwa zikikosewa na kutafsiriwa tofauti mara nyingi.  Hii ndio maana wengi wamekuwa hawatilii maanani na pia wengi kutopata matokeo halisi yanayotarajiwa.  Safu ya gazeti hili leo inakwenda kukufungua na kukusaidia.

Yafuatayo ni baadhi ya maeneo katika maisha yetu ya kila siku ambayo huleta matatizo kwa kushindwa kuwa na ujuzi wa kujisaidia wenyewe.

1.Unapokuwa Katika Hasira Kali.
Kama vile yalivyomatundu katika kuta kubwa kwa ajili ya kupumulia hewa na kupunguza presha  katika ukuta huo ili usije pata nyufa  (ventilations) ndivyo hivyo mtu mwenyehasira  kali hutakiwa kujua jinsi ya kuyaruhusu mazingira aliyopo yaweze kumsaidia kuipumulia nje ile hasira pasipo kuleta madhara kwake yeye na wale wanaomzunguka  ( venting anger )

Tumeona sana katika filamu au vitabu vya  asili ya nchi za magharibi wengi wakiwa katika hali hii hukumbatia au kung’ata au kupiga ngumi mito ya kulalia (pillow) au wengine hutupa ngumi katika mfuko wa mazoezi ya kupigana (punching bag) katika hali hii hasira kali hupata pakupenyezea na kupoa.  Watalaam wameshauri kutumia nguvu zote kutupa ngumi au kupiga mito hii au puching bag na kama ni mtu amekuudhi basi fikiria kuwa unauona uso wake katika mto huo na uiachie hasira yako kimwili (kwa kupiga)  na kimaneno kwa kuongea yale yote yaliyo moyoni mwako. Watafiti wanasema aina hii yaweza pia kuwa msaada kwa kupunguza msongo wa mawazao mbali na hasira.

Tafiti za hivi karibuni zimeonyesha mtazamo wa tofauti kidogo katika hili.  Dr Brad Bushman  mwanasaikolojia  wa Iowa state university anasema watu wengi hufikiri kwa kufanya hivi wanafanikiwa kupona hasira ila wale wachache ambao inashindikana wanakuwa na hasira kali maradufu na kuchanganyikiwa.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa kukosewa kwa namna ya kuipunguza au kuitoa hasira kumewasababishia wengi matatizo ya misuli ya kichwani na hivyo kuhatarisha akili zao.

Nini Kifanyike Basi
i)                    Jaribu kufanya chochote kile ambacho chaweza kikachukua nafasi ya hasira moyoni, kila mtu anakitu anachokipenda, kifanye hicho sasa, kwa mfano; kuangalia filamu, picha, kusoma au kusikiliza hadithi au kusikiliza nyimbo unazozipenda, jihadhari kukaa karibu na yule aliyekukwaza mpaka mmesuluhisha yaliyowasibu.
ii)                  Pata muda wa kucheka na marafiki wengine, kama ni baba pata muda wakutoka na watoto wako, hawa wananafasi kubwa ya kukuingia moyoni kwa haraka na kusafisha hasira uliyonayo.
iii)                Usikimbilie sana kwenye mazoezi ya viuongo kwasababu utafiti wa Dr. Bushman unaonyesha kuwa mazoezi ya viungo yananafasi kubwa ya kuiamsha hasira, wengi waliotafitiwa walienda kupigana mara tu baada ya kumaliza mazoezi ya viungo.
iv)                Michezo ya kijadi kama vile tai, chi, na yoga yaweza kuwa msaada wa kurekebisha hisia na hali ya akili, ni vema ukafanya michezo hii kama unaujuzi nayo na kama inaruhusiwa na imani yako, kwa sababu mingi iko zaidi katika imani za dini za  nchi za bara Asia.
v)                  Muendelezo wa kufanya kazi au shughuli itakayochukua muda mrefu wa kufikiri na kuifanya bize akili yako inaweza kupooza hasira pia.





2. Unapokuwa  Umefadhaika, Umepooza, Unahuzuni na Kuvunjika Moyo   
Tafuta sana kufikiria yale yaliyo mema na ya kukutia moyo.  Peleka moyo wako katika yale yanayokupa furaha zaidi kuliko katika yale yanayovunja furaha yako. Funga milango yako ya akili, usiruhusu chochote kisicho cha furaha kuingia ndani. Tumia ubongo wako kufikiri kuwa yote yanawezekana                   (optimistic thinking).

Teka uwezo wa akili na fikra zako na uzielekeze kule tu unakopenda wewe,
usiruhusu kamwe watu au mazingira yakuletee picha inayokuumiza moyo
Tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi tunapokuwa katika huzuni na kuvunjika moyo kila kitu huonekana kinyume nasi.  Nguvu ya ubongo nayo inashindwa kuyadidimiza yale yaliyo mabaya ili tusiyawaze.  Na kila tunapojaribu kujitahidi wenyewe kuikataa hali hii mawazo na mitazamo ya kufeli na kushindwa hujaza fikra zetu.  Mara unapojaribu kufikiri yale mema moto huwa mkali zaidi na kuona kuwa wewe ni wakushindwa zaidi.

Ufanye nini Basi?

i)                    Pata muda zungumza na marafiki, watu wa dini (wachungaji, mapadri, shekhe, washauri au yeyote anayeweza kukupa mitazamo ya tofauti na kukuwezesha kuwaza mambo mengine.
ii)                  Nenda katika maeneo ambayo watu wanafurahi, kama vile sherehe, ufukweni, hotelini, super market au katika maduka makubwa,  taratibu utaona roho na nafsi yako vinanyanyuka upya.
iii)                Na kama unajua kuwa kunakitu kitakuudhi na kuharibu furaha yako panga vitu vingi vilivyo vyema na vyakukujenga utumie muda kuviwaza hivyo.

3. Unapojihisi Kupoteza Mwelekeo wa Maisha

Kumbuka na uyafikirie tena na tena malengo yako, hii itakuwezesha kuyafanya yawe kweli. Pata mawazo na picha ya wewe ukifanikiwa na sio ukishindwa, iache picha hiyo ikae katika akili yako, itakusaidia kuyafanya matendo yako yapiganie uhalisi wa kile kilichopo akilini mwako.

Kuwaza tu kuwa unafanikiwa hakutoshi, hapa ninazungumza pia na wale wenye imani zao kali za dini ambao hukesha wakiamini wanafanikiwa na wamekwisha fanikiwa na wakati hakuna wanachokifanya, lazima ufanye mabadiliko yakimtazamo lasivyo kifo kitakukuta hapo hapo ukiwaza unafanikiwa wakati watu wanakuona wewe kama mfano mzuri wa walioshindwa maisha.  Lazima picha ulionayo ya kufanikiwa itiwenguvu na matendo(actions) ya kila siku katika kuifanya ndoto yako kuwa halisi “to make your dream come true”
Shelley Taylor, Daktari wa saikolojia wa chuo kikuu cha UCLA Marekani ameonyesha kuwa katika kufikiria tu kuwa unafanikiwa  na kuliwekea picha lengo lako katika akili bila matendo ina athari mbili; Kwanza inalitenganisha lile lengo mbali na kile kinachohitajika kufanywa ili lengo lifikiwe, na pili inakufanya ufurahie utamu wa kuwa mtu aliyefanikiwa wakati bado kabisa hujafika popote,  hali hizi zinafifisha nguvu ya lengo lako (power of the goal) na kukufanya kushindwa kujitahidi kufanya kazi na kukubali kupoteza (to take risks) katika kukipata kile ambacho kiko katika ndoto zako za kila siku.

Nini kifanyike?
i)                   Pamoja na kuwaza kila siku na kuwa na ndoto za mafanikio, pata wakati jiulize ninini unaweza kufanya ili kufikia mafanikio hayo, na ukipata njia au mbinu hizi anzia kuzifanyia mazoezi akilini kabla ya kuziweka katika uhalisia.
ii)                 Kwa malengo ya muda mfupi waweza kupitia hatua zote ulizo zipanga ndani ya siku moja kabla ya kuanza kuzitendea kazi.  Lakini kwa malengo makubwa na yamuda mrefu unaweza kupitia mipango yako tena na tena kadri unavyozidi  kuendelea na mchakato mzima na uone kama kunahitajika marekebisho.

4. Unapokuwa na hali ya Kutojithamini na Kutojipenda (Low Self Esteem)

Jitambue ya kuwa wewe ni wathamani na ni mtubora zaidi.  Hii itakuwezesha kujithamini na kujipenda. Jifunze kuandika maneno ya ushindi yanayoonyesha ujasiri na ukakamavu (affirmation) kwa mfano viko vikaratasi vidogo vya kunatisha (stickers) katika kuta au katika magari vinamaneno “every thing is possible” vikimaanisha kila kitu kinawezekana.  Nyingine zimeandikwa “I can do it’ (ninaweza), nakumbuka nimeona katika gari la rafiki yangu kikaratasi  cheye maneno ya dini “nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu” maneno haya na mengine mengi yawe ya dini au yakutungwa au waweza kuandika mwenyewe na kubandika katika ukuta wako, kioo cha kujitazama, katika mlango wa friji yako, ndani ya gari lako, pembeni ya kitanda au bafuni.  Kwa teknolojia ya sasa unaweza kuyarekodi maneno haya na yakasema katika redioyako mara kwa mara au kuyaandika  katika compyuta yako yakawekwa kama “screen saver”  ili mradi tu kila unapogeuka unayaona yanasema na wewe.  Maneno haya yana nguvu ya kupenyeza ujumbe ndani ya fikra na moyo wako na kuruhusu mwili wako kudaka na kuyatendea kazi.

William Swann, daktari wa chuoo kikuu cha Texas anasema mtazamo huu unaweza kuwa mgumu kidogo na sio wote wanaweza kufanikiwa katika hili kwasababu kubadili jinsi tunavyojihisi wenyewe ni kazi ngumu sana.
Hali ya kujithamini na kujipenda inategemea mambo mawili; Kwanza hisia zetu za jinsi gani tunavyojipenda, na pili hisia zetu za uwezo gani tulionao katika kazi zetu na shuhuli nyingine zinazohitaji ujuzi na vipawa vyetu. Katika hili matumizi ya maandishi  yanayoonyesha ushindi na kuweza (affirmations) yaweza kufanikiwa kwa baadhi ya watu lakini pale yanaposhidwa kufanya kazi huweza kumuacha mtu akiwa ameumia moyo zaidi.

Mara nyingi wale wenyemitazamo mibovu kuhusu wao wenyewe hawajiamini na hawaamini kama waweza kusema au kufanya  kitu bora hata siku moja kwa jinsi hii hata kama wakiandika vimaneno vingi vilivyo vya kutia moyo bado hawatakuwa na imani maana wanachokijua wao ni kwamba kamwe hakuna  chema kitakachoweza kutoka kwao. “Nothing good shall ever come from them”

Nini kifanyike basi?

i)          Njia pekee ya kubadilisha matunda ya vile tunavyojihisi au tunavyojithamini ni kubadili vile vinavyotuingia na kutengeneza  ile hali ya jinsi tunavyojiona. Kwamfano; kama unajikuta unashindwa kujithamini au kujipenda sababu ya wale unaohusiana nao   au unaokuwa nao zaidi, basi badilisha,chagua watu wengine wakuhusiana nao, labda hao watasema yaliyobora kuhusu wewe na kukutia moyo zaidi.  Kama uko katika ajira ambayo kila mtu anakuona wewe hujui na wewe niwakushindwa tu, amua kuwataka wabadili mtazamo wao kwako au ikibidi  ondoka pata kazi sehemu ambayo watu wanamtazamo mzuri kwako.  Jaribu kufanya kazi yako vema zaidi ya ulivyoifanya kule kwa awali.

ii)        Simama ujitetee mwenyewe usingoje kutetewa “stand for yourself”
hakikisha unazungukwa na watu wanaokuona kuwa wewe ni wathamani, unayeweza, na ni mtu mwema. Hakikisha wanalikiri hilo kwa vinywa vyao.Uwe mvumilivu na wakati wote jitahidi kutimiza majukumu yako ili usiwavunje moyo wale wanokuona wewe kuwa mtu mwema na wanayekuamini. Fahamu kuwa jinsi tunavyojiona sisi wenyewe, na mtazamo tulionao kuhusu sisi wenyewe (self esteem) ni mjumuisho wa jinsi tunavyohusiana na watu wanaotuzunguka kwa muda tuishio hapa  duniani na kwamwe hauwezi kubadilika kwa usiku mmoja.

5. Unatatizo la Mawasiliano Katika Mahusiano Uliyonayo:
Usikivu makini (active listening) unaweza kukusaidia kuwasiliana vema na rafiki yako au mpenzi wako. Katika usikivu makini tunamaanisha sio tu kusikia, bali kuelewa kwa uhakika kile mwenzako anachojaribu kukisema.  Hapa ndipo tofauti kati ya neno “hearing” na neno “listening” inapojidhihirisha na hata maneno kusikia na kusikiliza yanapoonyesha tofauti.  Katika mahusiano baina ya watu, marafiki, wapenzi, ni lazima kuwepo na kusikilizana “listening” na sio “kusikiana”
            Mahusiano mengi na hata ndoa nyingi zimekuwa na migogoro na hata mivunjiko maana kumekuwa na kusikiana zaidi ya kusikilizana kamwe msisahau kuwa tunayasikia magari, tunasikia ndege wa angani na ndege za abiria, tunasikia upepo na miti na makelele mengine lakini tunawa sikiliza watu  na yale wanayoyasema.

Tunasikiliza kile tunachoelezwa kwa kukitathmini kama vile kilivyosemwa na tunakirudia kwa maneno yetu wenyewe tukijaribu kifikiri kile mwenzetu anachojaribu kutuambia.  Katika hili tunatambua yakwamba kusikiliza ni mchakato (process) wakati sio hivyo katika kusikia. Baadhi ya wachunguzi wamegundua kwamba usikivu makini au masikilizano, yanawasaidia zaidi wale walioko katika mahusiano mazuri, lakini maranyingi mchakato mzima wa kusikilizana hukwama hasa pale wapenzi wanapokuwa katika ugomvi au mahojiano makali, hapa kusikilizana huwa ni ndoto.


Zingatia haya!

 Walioko katika mahusiano (wanandoa) wajaribu  kupeleka jitihada zao zote katika mambo matatu muhimu

i)                    wanawake wajitahidi kuwasilisha hoja na madai yao katika hali ya upole na upendo. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume wengi wamekuwa tayari kusikiliza toka kwa wanawake pale ambapo wanaongeleshwa kwa utulivu na unyenyekevu.

ii)                  Wanaume wanahitaji kuwasikiliza wenza wao kiufasaha na kuzingatia juu ya hisia na mawazo yao.

iii)                Pande zote mbili yaani wanaume na wanawake jitahidini kwa kila hali kuutuliza utu wa kiume na kuutiisha.  Kiasili wanaume wanatabia ya kuhemka nakuwaka hisia zao za hasira haraka hasa wanapogadhibishwa, na kwa hali hii hujitahidi kujitoa kwenye tatizo haraka ili waziponye nafsi zao hatakama ufumbuzi wa tatizo haujapatikana na hii hufanya matatizo mengi katika mahusiano kuachwa bila suluhisho “unsolved Conflicts” na hali hii pia huwaacha wanawake katika hasira na maumivu makali.

Jitahidini kuhakikisha hamfikii katika hali hii kwa kurushiana utani kidogo au mwanamke kumkumbatia mwanaume angalau kupunguza gadhabu yake na mara mtajikuta mnaishia pazuri.  

Saturday, January 19, 2013

Je Mkristo Anaweza Kuwa Na Maumivu Ya Ndani?

Je Mkristo Anaweza Kuwa Na Maumivu Ya Ndani??? 

 Ukisoma katika Luka sura ya 4 utaona kuwa Yesu anaongelea watu wenye majeraha ya ndani. Anaanza kwa Kusema Roho wa Bwana Yu Juu yangu Kwa maana amaenipaka Mafuta....na Kuendelea. Ukisoma hapo pamoja na references zake utaona kuwa Yesu anaongelea pia majeraha ya ndani. Anaeleza kuwa katika Ujio wake pia amekuja kuwaganga waliovunjika moyo. Alijua yapo majeraha ndo maana akayaongelea.
Wote tunajua jeraha ni nini, kifupi ni maumivu yanayobaki kwenye mwili wa mwanadamu baada ya kujeruhiwa kwenye mwili. Unaweza ukamuona mtu yuko mzima lakini ukibonyeza penye jeraha huyu mtu atatoa ukelele mkubwa pengine mpaka machozi. Yamkini unaweza kumuona mwanamke mzuri, ama mkaka handsome, unaweza muona mtu yupo na furaha kumbe ana jeraha la ndani, huwezi mjua kwa kumtazama ila kwa kugusa pale alipowahi umizwa maishani mwake.
1. Hivi Mkristo ana Maumivu ya Moyo?
Jibu Mkristo anayo maumivu ya moyo ingawa hapaswi kuishi nayo, watu kuumia wanaumia
lakini hupaswi kuishi kwenye hayo maumivu. Mwandishi wa Zaburi anaandika Kwanini Nafsi Yangu kuinama? Hii yote ni kuona kuna wakati tunakuwa na maumivu ya moyo huwa yanatokea, lakini unapaswa umuombe Mungu usiishi katika hayo.Wakristo ni Wanadamu kama walivyo Wanadamu wengine.
Kuna watu wengi sana wana maumivu ya Moyo lakini hawajui kama wanamaumivu ya moyo kwenye maisha yao. Assume ulikuwa unafanya kazi kwenye Kampuni fulani labda Marafiki Huru Company, baada ya muda ukafukuzwa kazi, sasa ukitaka kujua una maumivu yasiyokuwa na hisia ni once unapokuwa umesikia habari njema ama mbaya za ile kampuni ndani ya moyo wako unajisikiaje ukiona unafurahia kuangamia kwake na kukasirika mafanikio yake basi jua unajeraha na jeraha la nafsi unapaswa uliepusha ndani yako.
Kuna Njia kama Tano za kubaini Mtu mwenye Jeraha ndani yake.

1. Kutokutaka Kuona/Kusikia Kuhusu kitu kilichomletea Jeraha-
Kama umewahi kuwa na majeraha yanayotokana na mahusiano, basi utakuta haupendi kusikia chochote
kinachomuhusu mwenzi wako wa zamani. Kama ni Kanisa hupendi sana kusikia habari zao unaamini wewe kuwa salama ni kujiepusha nao lakini once akitokea Yule mpenzi wako ghafla mmekutana mlimani city, moyo wako unararuka na unajikuta unatafuta njia ya kupita
ujiepushe nae. Ama kama unaona muito wa simu na kuangalia simu yako na kugundua ni mtu alijekujeruhi kwa namna moja ama nyingine, ukishaona unaanza kujipanga na kukunja uso kabla hujapokea na kuna fundo linakushika shingoni basi jua "Hayajaisha" hata kama unajikausha kwa kiwango gani.
2. Kupenda kusikia habari mbaya za Mtu/Kundi ama Jumuiya iliyokuletea Majeraha-
Unajisikiaje ndani ya nafis yako pale unaposikia mtu aliyeujeruhi moyo wako amepata ajali?moyoni unasema kisasi ni cha Bwana??au unasema Malipo ni hapa hapa duniani??ukiona
moyo wako unajisikia kupona unapopata habari mbaya kutoka kwa jamaa aliyekujeruhi
basi jua una jeraha ndani. Assume ungekuwa bado mna uhusiano wowote then baya lingetokea ungejisikiaje?
3. Kujihami/kuchukua tahadhari kutokana na jambo hilo-
Kama umewahi kutana na mdada ambaye amejeruhiwa nafsi yake kwenye mahusiano, ukianza kumfukuzia cha kwanza anachojiandaa ni kuto kuumia tena, ukimwambia kuhusu mahusiano anakuwa mkali, utaona ana kutumia sms kali sana SITAKI MAHUSIANO NA WAKAKA au utasikia "FOR NOW AM NOT INTERESTING WITH MEN" kwa sisi wataalam tunajua hii ni defence ya kuogopa kuguswa kidonda. Sasa kuna kasheshe ya kudate mdada ama mkaka
aliyewahi umizwa, njia nyepesi kwanza tibia jeraha kabla hujapanda kwenye moyo wake, vunja madhabahu za awali kisha jenga mpya, uki-ignore I tell you itakula kwako.
4. Chuki na Hasira Juu ya Chochote chenye kumletea Kumbukumbu ya zamani- Utakuta mtu kama ana picha anachoma moto kama ni nguo anachoma kama ni mtaa ndo umemsababishia hilo tatizo anahama, kama ni Kanisa ama mchungaji hataki kumuona. Ukimtazama hivi anakuwa kama yuko normal lakini kama mkapita sehemu ambayo imemsababishia jeraha unaweza kukuta ANASONYA ukimuuliza utasikia walaaa am just Ok. Kama kuna watu wanamsifia Mchumba wako waliyekujeruhi ama mtu aliyekuzima hela zako Kuna FUNDO la hasira huja kukaa kwenye koo, yaani unatamani umchane chane huyo mtu kama yuko mbele yako, unajikuta hutaki kukasirika lakini ndo unalo. Umewahi Kukutana na Mtu ambaye aliwahi pata ajali sehemu fulani ikatokea kila akipita eneo hilo anasisimka mwili mzima mpaka nywele zinasimama
5. Kupenda Kujitenga-
Mtu yeyote mwenye Jeraha anataka kukaa peke yake akiamini yeye ndo yuko salama. Unaweza kuta mtu mlizoea kuwa nae kwenda outing, mlizoea kuwa pamoja kabla ya kupata jeraha la nafsi mwisho wa siku unakuta mtu anabadilika, anatamani kukaa peke yake. Popote anaposikia "mbaya" wake yupo salama yake yeye ni kuto kukaa na huyo mtu ama group la hao watu. Hujawahi kumuona mtu mlikuwa kwenye Kamati Fulani pengine kutokana na Maneno ya Watu ama Yanayoendelea huyu mtu ghafla anatangaza "Kupumzika" kuwa mwana kamati, mnatafuta sababu hamuoni mkimuuliza anasema am just ok napumzika kwanza, basi jua katika sehemu ya ndani ya huyu mtu imeguswa na heri na salama kwake ni Kukaa mbali na nyie. Mpaka Jereha likitulia atawatafuta tena.
2. Je Ni Dhambi ukiwa na Maumivu?
Kwa maelezo niliyoyatoa hapo juu kwangu Mimi kwa Mkristo kuwa na maumivu PASIPO kuyashughulikia kwake ni dhambi. Na mbinguni haendi (Black and White). Kama mwenyewe huwezi unapaswa kusaidiwa namna ya kuachilia.
Maomivu ya ndani usipo yashughulikia yana develop tabia, na tabia inayokuwa developed haina tabia za kiungu ndani yake, nilizozitaja hapo juu ni baadhi tu ya Tabia zinazokuwa developed mtu anapokuwa ameumizwa. Kuna baadhi ya dhambi huzaliwa mtu anapokuwa na msongo wa mawazo na akaamua kujitenga na watu. Mojawapo ya tabia hizo ni mtu kuamua kulewa ili kuondoa mawazo, nimewaona marafki zangu kadha wa kadha walianza kunywa pombe sababu tu wanataka kufuta kumbukumbu mbaya walizonazo kuhusu ajira, dhuruma, mapenzi na hata uhusiano wa ndugu. Nimewaona watu wameanza kufanya ngono kupita maelezo sababu wamekuwa wakitafuta amani ya nafsi. Ndio maana Biblia inasema 'Njooni Kwangu Ninyi Nyote wenye Kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha". Kuna watu wamefikia hatua ya kujiua ama kuwaza kujiua baada ya kuona hakuna tumaini tena kwenye maisha yao.

Nimewahi wasaidia wengi (Wale waliotaka Msaada kwa Maana halisi, yaani WALIOLEMEWA na kutaka kutua mzigo kuna wengine wanalemewa lakini wanajikaza, kuna wengine ambao mizigo yao ni mikubwa zaidi nimewashauri wapeleke kwa watu wazima zaidi ama wachungaji wao. Kwa Umri huu nilionao na hekima chache ambazo Mungu amenipa nimekaa sana sana na Wanandoa Marafiki zangu kusaidia namna moja ama nyingine kunusuru. Lakini katika Yote nilipofanya uchunguzi kwenye baadhi ya Kesi nimegundua kuna mambo kama Matatu kwa Wanandoa.

i. Hawakutumia Muda Mwingi Kujenga Urafiki Wao Kwanza. Mtu anaolewa na Mtu mwingine hana a,b,c za kutosha kuhusu huyo Mtu. Biblia katika Zaburi 11:3 inasema Kama "Kama Msingi Ukiharibika Mwenye haki atafanya Nini"???
ii. Athari za Makuzi na Malezi--Kwa Kuwa watu hawakuwa marafiki hawakuwa na muda pia wa kusoma Personalities zao. Tumeathiria sana namna tulivyolelewa. Namna ya Kupenda na kupendwa inategemea sana na ulivyo lelewa. Kuna wengine wamelelewa kuonesha mapenzi hadharani maana baba yake na mama yake walikuwa wanapigana mabusu sebuleni, baba anamsifia mama, lakini sasa unakuta kuna mwanaume hawezi kabisa mambo hayo kwake mapenzi ni jambo la siri sana. Kama Umeolewa ama Umeoa mtoto ambaye ni wa mwisho kuzaliwa, ama wa kwanza kuzaliwa basi jua wana tabia tofauti, watoto wengi sana wa mwisho kuzaliwa wamezoea kufanyiwa maamuzi, na watoto wa kwanza wamezoea kufanya maamuzi wenyewe, ama ukiwa na mtu ambaye amezaliwa peke yake kwenye familia yao, ama mtu aliyekulia na bibi yake ni tofauti na ambaye alipokuwa mdogo wazazi wake walifariki na akaamua kujitafutia maisha, kuna watu wanaamini maisha ni kufight na kuna watu wanaamini maisha ni Network ya watu.
iii. Expectations ---Ukiwa na uhusiano na Mkaka aliyekuwa Player, na Ukiwa na Mdada ambaye alikuwa hajawahi kuwa na uhusiano hata mmoja, expectations ndani ya ndoa zinatofautiana sana. Wengi wa Wanandoa Wanaingia kwenye ndoa wakiwa na 'High Expectations za Kuwa Loved", ndio maana kesi nyingi nilizokutana nazo utasikia, "Mimi nilitegemea yeye kama Mke, ajue hili" na "Mwngine nasema Nilijua yeye kama Mume aaamue", mwisho wa siku unakuta "High Expectations" zinapelekea "High Disappointments". Kuna wanaume kwenye ndoa neno "Asante", "Samahani", "nimeelewa" kwao ni misamiati. Kuna mambo madogo madogo sana yanayojenga ndoa. Unakuta Mkeo anakuambia "Umependeza" wewe unachukulia poa, ama "Pole na Kazi" wee unasema asante huku unaenda chumbani, unaambiwa tabia hii na hii sio nzuri unasema "ndo nilivyo".
Changamoto ni nyingi sana lakini hazizuiii wengine kuingia huko kwenye ndoa
.
Nini Kifanyike Unapokuwa Umeumizwa Moyo Wako.....Read Me Next Episode.


Kwa Msaada Zaidi tuwasiliane.

+255767006454

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Marufu Tanzania

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Maarufu Tanzania

Mungu ameibariki Tanzania Kwa Kila aina ya Baraka za Mwilini na rohoni. Leo na wiki chache zijazo nitakujuza Watumishi 25 ambao ukiwataja kwenye mikoa zaidi ya Kumi hapa Tanzania yamikini wameshasikika na unaweza pata comments toka kwa waumini wao. Kuna Makanisa ambayo pengine yamesikika zaidi kuliko kuliko majina ya watumishi hao ama kuna watumishi wamesikika zaidi kuliko hata Makanisa wanayochunga.

Kuna Watumishi ambao wamekuwa maarufu sababu ya huduma zao kwa Ujumla, Sababu utajiri wao, sababu za huduma zao kwa wanafunzi ama kwa program zao za mahali pamoja.

lengo la Makala haya si kutafuta nani yuko Juu zaidi ya mwingine ila kutoa taarifa kwa umma na kuwatia moyo watumishi hawa kuwa kazi yao imevuka mipaka ya mikoa na nchi.

Tahadhari
Yawezekana vigezo vyako sio vugezo vyangu katika kuwasilisha.

Apostle Maboya(Ni kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania

Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini


Mwalimu Christopher Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya New Life Crusade/ New Life in Christ.



Mchungaji Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.



Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.




Mtume Veron Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.


Askofu Moses Kulola wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila kona ya Tanzania

Nabii GeorDavie wa GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.

Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.


Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM) na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.

ni hao kwa leo tutaendelea kukujuza zaidi endelea kufuatilia