MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

Tuesday, February 19, 2013

MATOKEO YA FORM FOUR 2012 HAYA HAPA

60% ya wanafunzi wafeli mtihani
MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.

“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.

 

BONYEZA (BOFYA)HAPA MATOKEO YA FORM FOUR 2012(hosted by lafa)


BONYEZA HAPA KWA QT RESULTS

2 comments:

  1. ndugu zanguni hebu tujaribu kufikiria hata kama mishahara kwa waalimu haitoshi hivi haya matokeo ni bayana?????

    ReplyDelete
  2. Kwangu naona sio bayana kabsa hebu unajua Tanzania Siasa imeingilia kati sana swala la Elimu kitu ambacho ni hatari kubwa sana

    ReplyDelete

YOUR WORMY WELCOME TO SAY ANYTHING TO ME IN MY WEBSITE