MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

Sunday, January 6, 2013

UNAWEZA KUPUNGUZA UNENE KWA KULA VYAKULA VIFUATAVYO



NI ndoto ya WATU WENGI wengi wanene kupunguza unene, lakini wengi wao hawajui wafanye nini. Zipo njia nyingi za kumfanya mtu apunguze unene, miongoni mwa njia hizo ni pamoja na vyakula, kujua aina ya vyakula unavyotakiwa kula na kuvila kama inavyoelekezwa.
Tikitimaji.
Vifuatavyo ni vyakula, mboga na matunda ambayo yakiliwa kwa mpangilio mzuri huondoa mafuta ya ziada mwilini na hivyo kupunguza unene wa ziada. Vyakula hivi vina sifa ya kuchoma yenyewe mafuta kabla ya kuhifadhiwa mwilini:


Machungwa.
MATUNDA
Matunda ni miongoni mwa vyakula vinavyoyeyusha mafuta mwilini, idadi kubwa ya mtunda huwa na kiwango kidogo cha kalori (calories) lakini yana kiasi kingi cha kamba lishe (fibre).
Matunda yenye kamba lishe nyingi huyeyusha mafuta mwilini haraka kwa kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na humuongezea mtu nishati ya mwili. Kwa sababu hii, unaweza kuchanganya ulaji wa matunda na vyakula vyenye mafuta bila kuongezeka unene. Matunda kama epo, machungwa, zabibu, mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiasi kingi cha kamba lishe.

Mapera.
Vilevile, tikitimaji lina faida kubwa mwilini, kwani lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini (toxins) ambayo huingia mwilini kwa njia ya chakula na hewa tunayoivuta kutokana na hali halisi ya maisha ilivyo. Pia tikitimaji linapoliwa huondoa maji ya ziada mwilini, pendelea kula tikitimaji kila wakati unaposikia tumbo kujaa au kuchafuka.
KABEJI
MBOGA ZA MAJANI
Mboga nyingi za majani huwa na kiasi fulani cha kamba lishe, na kamba lishe iko katika makundi mawili, ya kwanza ikiwa ni ile inayoyeyuka mapema na ile isiyoyeyuka mapema, mbogamboga zinazochukua muda kuyeyuka tumboni lakini zinasaidia sana usagaji wa chakula haraka ni pamoja na mchicha, spinachi, kabeji, maharage ya kijani na nyingine jamii ya majani kibichi.

PROTINI
Idadi kubwa ya vyakula vinavyoyeyusha mafuta haraka mwilini katika jamii ya vyakula vya protini ni vyakula vya baharini. Ingawa samaki huhitaji nishati nyingi kuyeyushwa mwilini, lakini ni miongoni mwa vyakula vinavyosaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini kwa haraka zaidi. Ili kupata matokeo mazuri na ya haraka, pendelea kula vyakula vya baharini sambamba na mboga za majani kama vile kabichi au saladi ya mbogamboga mchanganyiko.
Vilevile kuna aina nyingine ya vyakula ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuyeyusha mafuta ya ziada mwilini kama vile vyakula vitokanavyo na maziwa, ngano isiyokobolewa, wali, ambavyo wakati wa kutayarisha unatakiwa kuhakikisha vinakuwa na kiwango kidogo cha mafuta asilia bila kuongezewa ya ziada. Ukizingatia ulaji wa vyakula vilivyoanishwa hapo juu kwa wingi, bila shaka utapungua mwili au hutaongezeka mwili zaidi ya ulivyo sasa.

MBEGU ZA MABOGA ZINA UWEZO WA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 10 HATARI



ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
UGONJWA WA MOYO
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia (magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha  usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.
KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
MAFUTA YA OMEGA -3
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.
KIBOFU CHA MKOJO
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.
KINGA DHIDI YA SARATANI
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
UGONJWA WA KISUKARI
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.
AFYA YA MOYO NA MAINI
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.
DAWA YA USINGIZI
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri na tulivu.
DAWA YA UVIMBE
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu.

KANUNI BORA ZA USALAMA WA KOMPUTA




Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.Kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
Mazingatio.
  • 1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
  • 2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
I.Tumia programu za uhakika
 Je umewahi kujiuliza kwanini natumia programu hii badala ya ile? Ukuaji wa teknolojia umesababisha kila mtu kuja na programu yake,kuna zile za bire,za kugawana na hata zile za bei chee.Sasa sitaki kusema kuwa programu za bei ya juu ndio bora au zile za bei ya chini ni za kukimbiwa kama ukoma,ila wewe kama mtumiaji unatakiwa kufanya kautafiti kadogo kabla ya kuamua kutumia programu fulani. Siku hizi kuna google ambayo inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya utafiti na kuangalia maoni ya watumiaji juu ya programu husika.
 Kwa kufanya hivi itakusaidia unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na kuleta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha wengi. Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
II.Hakikisha unajua nini unachokifanya
 Wengi wetu tumekuwa wahanga kutokana na kukubali kiholela au kufanya mambo tusiyoyajua.Labda nikupe mfano mmoja wa mtu wangu wa karibu ambaye aliwahi kuvamiwa na na hizi programu za matangazo(Adware).Yeye alikuwa alifungua tovuti moja mara akaona ujumbe unasema kompyuta yako ipo hatarini hivyo bonyeza hapa ili kutatua.Bila kujua anachokifanya akabofya na kujikuta ameshaingiza madudu kibao.
 Hivyo kuwa makini kila unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
Hayo ni mabo machache ambayo unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye kinga bora.