MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

Saturday, January 19, 2013

Je Mkristo Anaweza Kuwa Na Maumivu Ya Ndani?

Je Mkristo Anaweza Kuwa Na Maumivu Ya Ndani??? 

 Ukisoma katika Luka sura ya 4 utaona kuwa Yesu anaongelea watu wenye majeraha ya ndani. Anaanza kwa Kusema Roho wa Bwana Yu Juu yangu Kwa maana amaenipaka Mafuta....na Kuendelea. Ukisoma hapo pamoja na references zake utaona kuwa Yesu anaongelea pia majeraha ya ndani. Anaeleza kuwa katika Ujio wake pia amekuja kuwaganga waliovunjika moyo. Alijua yapo majeraha ndo maana akayaongelea.
Wote tunajua jeraha ni nini, kifupi ni maumivu yanayobaki kwenye mwili wa mwanadamu baada ya kujeruhiwa kwenye mwili. Unaweza ukamuona mtu yuko mzima lakini ukibonyeza penye jeraha huyu mtu atatoa ukelele mkubwa pengine mpaka machozi. Yamkini unaweza kumuona mwanamke mzuri, ama mkaka handsome, unaweza muona mtu yupo na furaha kumbe ana jeraha la ndani, huwezi mjua kwa kumtazama ila kwa kugusa pale alipowahi umizwa maishani mwake.
1. Hivi Mkristo ana Maumivu ya Moyo?
Jibu Mkristo anayo maumivu ya moyo ingawa hapaswi kuishi nayo, watu kuumia wanaumia
lakini hupaswi kuishi kwenye hayo maumivu. Mwandishi wa Zaburi anaandika Kwanini Nafsi Yangu kuinama? Hii yote ni kuona kuna wakati tunakuwa na maumivu ya moyo huwa yanatokea, lakini unapaswa umuombe Mungu usiishi katika hayo.Wakristo ni Wanadamu kama walivyo Wanadamu wengine.
Kuna watu wengi sana wana maumivu ya Moyo lakini hawajui kama wanamaumivu ya moyo kwenye maisha yao. Assume ulikuwa unafanya kazi kwenye Kampuni fulani labda Marafiki Huru Company, baada ya muda ukafukuzwa kazi, sasa ukitaka kujua una maumivu yasiyokuwa na hisia ni once unapokuwa umesikia habari njema ama mbaya za ile kampuni ndani ya moyo wako unajisikiaje ukiona unafurahia kuangamia kwake na kukasirika mafanikio yake basi jua unajeraha na jeraha la nafsi unapaswa uliepusha ndani yako.
Kuna Njia kama Tano za kubaini Mtu mwenye Jeraha ndani yake.

1. Kutokutaka Kuona/Kusikia Kuhusu kitu kilichomletea Jeraha-
Kama umewahi kuwa na majeraha yanayotokana na mahusiano, basi utakuta haupendi kusikia chochote
kinachomuhusu mwenzi wako wa zamani. Kama ni Kanisa hupendi sana kusikia habari zao unaamini wewe kuwa salama ni kujiepusha nao lakini once akitokea Yule mpenzi wako ghafla mmekutana mlimani city, moyo wako unararuka na unajikuta unatafuta njia ya kupita
ujiepushe nae. Ama kama unaona muito wa simu na kuangalia simu yako na kugundua ni mtu alijekujeruhi kwa namna moja ama nyingine, ukishaona unaanza kujipanga na kukunja uso kabla hujapokea na kuna fundo linakushika shingoni basi jua "Hayajaisha" hata kama unajikausha kwa kiwango gani.
2. Kupenda kusikia habari mbaya za Mtu/Kundi ama Jumuiya iliyokuletea Majeraha-
Unajisikiaje ndani ya nafis yako pale unaposikia mtu aliyeujeruhi moyo wako amepata ajali?moyoni unasema kisasi ni cha Bwana??au unasema Malipo ni hapa hapa duniani??ukiona
moyo wako unajisikia kupona unapopata habari mbaya kutoka kwa jamaa aliyekujeruhi
basi jua una jeraha ndani. Assume ungekuwa bado mna uhusiano wowote then baya lingetokea ungejisikiaje?
3. Kujihami/kuchukua tahadhari kutokana na jambo hilo-
Kama umewahi kutana na mdada ambaye amejeruhiwa nafsi yake kwenye mahusiano, ukianza kumfukuzia cha kwanza anachojiandaa ni kuto kuumia tena, ukimwambia kuhusu mahusiano anakuwa mkali, utaona ana kutumia sms kali sana SITAKI MAHUSIANO NA WAKAKA au utasikia "FOR NOW AM NOT INTERESTING WITH MEN" kwa sisi wataalam tunajua hii ni defence ya kuogopa kuguswa kidonda. Sasa kuna kasheshe ya kudate mdada ama mkaka
aliyewahi umizwa, njia nyepesi kwanza tibia jeraha kabla hujapanda kwenye moyo wake, vunja madhabahu za awali kisha jenga mpya, uki-ignore I tell you itakula kwako.
4. Chuki na Hasira Juu ya Chochote chenye kumletea Kumbukumbu ya zamani- Utakuta mtu kama ana picha anachoma moto kama ni nguo anachoma kama ni mtaa ndo umemsababishia hilo tatizo anahama, kama ni Kanisa ama mchungaji hataki kumuona. Ukimtazama hivi anakuwa kama yuko normal lakini kama mkapita sehemu ambayo imemsababishia jeraha unaweza kukuta ANASONYA ukimuuliza utasikia walaaa am just Ok. Kama kuna watu wanamsifia Mchumba wako waliyekujeruhi ama mtu aliyekuzima hela zako Kuna FUNDO la hasira huja kukaa kwenye koo, yaani unatamani umchane chane huyo mtu kama yuko mbele yako, unajikuta hutaki kukasirika lakini ndo unalo. Umewahi Kukutana na Mtu ambaye aliwahi pata ajali sehemu fulani ikatokea kila akipita eneo hilo anasisimka mwili mzima mpaka nywele zinasimama
5. Kupenda Kujitenga-
Mtu yeyote mwenye Jeraha anataka kukaa peke yake akiamini yeye ndo yuko salama. Unaweza kuta mtu mlizoea kuwa nae kwenda outing, mlizoea kuwa pamoja kabla ya kupata jeraha la nafsi mwisho wa siku unakuta mtu anabadilika, anatamani kukaa peke yake. Popote anaposikia "mbaya" wake yupo salama yake yeye ni kuto kukaa na huyo mtu ama group la hao watu. Hujawahi kumuona mtu mlikuwa kwenye Kamati Fulani pengine kutokana na Maneno ya Watu ama Yanayoendelea huyu mtu ghafla anatangaza "Kupumzika" kuwa mwana kamati, mnatafuta sababu hamuoni mkimuuliza anasema am just ok napumzika kwanza, basi jua katika sehemu ya ndani ya huyu mtu imeguswa na heri na salama kwake ni Kukaa mbali na nyie. Mpaka Jereha likitulia atawatafuta tena.
2. Je Ni Dhambi ukiwa na Maumivu?
Kwa maelezo niliyoyatoa hapo juu kwangu Mimi kwa Mkristo kuwa na maumivu PASIPO kuyashughulikia kwake ni dhambi. Na mbinguni haendi (Black and White). Kama mwenyewe huwezi unapaswa kusaidiwa namna ya kuachilia.
Maomivu ya ndani usipo yashughulikia yana develop tabia, na tabia inayokuwa developed haina tabia za kiungu ndani yake, nilizozitaja hapo juu ni baadhi tu ya Tabia zinazokuwa developed mtu anapokuwa ameumizwa. Kuna baadhi ya dhambi huzaliwa mtu anapokuwa na msongo wa mawazo na akaamua kujitenga na watu. Mojawapo ya tabia hizo ni mtu kuamua kulewa ili kuondoa mawazo, nimewaona marafki zangu kadha wa kadha walianza kunywa pombe sababu tu wanataka kufuta kumbukumbu mbaya walizonazo kuhusu ajira, dhuruma, mapenzi na hata uhusiano wa ndugu. Nimewaona watu wameanza kufanya ngono kupita maelezo sababu wamekuwa wakitafuta amani ya nafsi. Ndio maana Biblia inasema 'Njooni Kwangu Ninyi Nyote wenye Kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha". Kuna watu wamefikia hatua ya kujiua ama kuwaza kujiua baada ya kuona hakuna tumaini tena kwenye maisha yao.

Nimewahi wasaidia wengi (Wale waliotaka Msaada kwa Maana halisi, yaani WALIOLEMEWA na kutaka kutua mzigo kuna wengine wanalemewa lakini wanajikaza, kuna wengine ambao mizigo yao ni mikubwa zaidi nimewashauri wapeleke kwa watu wazima zaidi ama wachungaji wao. Kwa Umri huu nilionao na hekima chache ambazo Mungu amenipa nimekaa sana sana na Wanandoa Marafiki zangu kusaidia namna moja ama nyingine kunusuru. Lakini katika Yote nilipofanya uchunguzi kwenye baadhi ya Kesi nimegundua kuna mambo kama Matatu kwa Wanandoa.

i. Hawakutumia Muda Mwingi Kujenga Urafiki Wao Kwanza. Mtu anaolewa na Mtu mwingine hana a,b,c za kutosha kuhusu huyo Mtu. Biblia katika Zaburi 11:3 inasema Kama "Kama Msingi Ukiharibika Mwenye haki atafanya Nini"???
ii. Athari za Makuzi na Malezi--Kwa Kuwa watu hawakuwa marafiki hawakuwa na muda pia wa kusoma Personalities zao. Tumeathiria sana namna tulivyolelewa. Namna ya Kupenda na kupendwa inategemea sana na ulivyo lelewa. Kuna wengine wamelelewa kuonesha mapenzi hadharani maana baba yake na mama yake walikuwa wanapigana mabusu sebuleni, baba anamsifia mama, lakini sasa unakuta kuna mwanaume hawezi kabisa mambo hayo kwake mapenzi ni jambo la siri sana. Kama Umeolewa ama Umeoa mtoto ambaye ni wa mwisho kuzaliwa, ama wa kwanza kuzaliwa basi jua wana tabia tofauti, watoto wengi sana wa mwisho kuzaliwa wamezoea kufanyiwa maamuzi, na watoto wa kwanza wamezoea kufanya maamuzi wenyewe, ama ukiwa na mtu ambaye amezaliwa peke yake kwenye familia yao, ama mtu aliyekulia na bibi yake ni tofauti na ambaye alipokuwa mdogo wazazi wake walifariki na akaamua kujitafutia maisha, kuna watu wanaamini maisha ni kufight na kuna watu wanaamini maisha ni Network ya watu.
iii. Expectations ---Ukiwa na uhusiano na Mkaka aliyekuwa Player, na Ukiwa na Mdada ambaye alikuwa hajawahi kuwa na uhusiano hata mmoja, expectations ndani ya ndoa zinatofautiana sana. Wengi wa Wanandoa Wanaingia kwenye ndoa wakiwa na 'High Expectations za Kuwa Loved", ndio maana kesi nyingi nilizokutana nazo utasikia, "Mimi nilitegemea yeye kama Mke, ajue hili" na "Mwngine nasema Nilijua yeye kama Mume aaamue", mwisho wa siku unakuta "High Expectations" zinapelekea "High Disappointments". Kuna wanaume kwenye ndoa neno "Asante", "Samahani", "nimeelewa" kwao ni misamiati. Kuna mambo madogo madogo sana yanayojenga ndoa. Unakuta Mkeo anakuambia "Umependeza" wewe unachukulia poa, ama "Pole na Kazi" wee unasema asante huku unaenda chumbani, unaambiwa tabia hii na hii sio nzuri unasema "ndo nilivyo".
Changamoto ni nyingi sana lakini hazizuiii wengine kuingia huko kwenye ndoa
.
Nini Kifanyike Unapokuwa Umeumizwa Moyo Wako.....Read Me Next Episode.


Kwa Msaada Zaidi tuwasiliane.

+255767006454

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Marufu Tanzania

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Maarufu Tanzania

Mungu ameibariki Tanzania Kwa Kila aina ya Baraka za Mwilini na rohoni. Leo na wiki chache zijazo nitakujuza Watumishi 25 ambao ukiwataja kwenye mikoa zaidi ya Kumi hapa Tanzania yamikini wameshasikika na unaweza pata comments toka kwa waumini wao. Kuna Makanisa ambayo pengine yamesikika zaidi kuliko kuliko majina ya watumishi hao ama kuna watumishi wamesikika zaidi kuliko hata Makanisa wanayochunga.

Kuna Watumishi ambao wamekuwa maarufu sababu ya huduma zao kwa Ujumla, Sababu utajiri wao, sababu za huduma zao kwa wanafunzi ama kwa program zao za mahali pamoja.

lengo la Makala haya si kutafuta nani yuko Juu zaidi ya mwingine ila kutoa taarifa kwa umma na kuwatia moyo watumishi hawa kuwa kazi yao imevuka mipaka ya mikoa na nchi.

Tahadhari
Yawezekana vigezo vyako sio vugezo vyangu katika kuwasilisha.

Apostle Maboya(Ni kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania

Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini


Mwalimu Christopher Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya New Life Crusade/ New Life in Christ.



Mchungaji Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.



Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.




Mtume Veron Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.


Askofu Moses Kulola wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila kona ya Tanzania

Nabii GeorDavie wa GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.

Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.


Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM) na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.

ni hao kwa leo tutaendelea kukujuza zaidi endelea kufuatilia