MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

MWL MTAKA



"KWA JINSI MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU HATA AKAMTOA MWANA WAKE WA PEKEE ILI KWA YUE AAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE"
SEMINA NA MIKUTANO MBALIMBALI INAPATIKANA HAPA

SOMO: KUTEKA BARAKA ZA MUNGU

MWANDISHI: LAMECK A MTAKA

MTUNZI: LAMECK A MTAKA

MAWASILIANO: +255786/0767 ---006454

EMAIL ADRESS :mtaka_2007@yahoo.com

UTANGULIZI
Ashukuriwe mungu awezae kufanya makuu kuliko yale tuwazayo mungu amekuwa nguzo katika maisha yangu yote yeye amekuwa akinitumia sehemu mbalimbali katika huduma yake na nimemuona akiponya na kuokoa watu katika huduma zangu mie nilizaliwa mwanza wilayani Geita na nilisoma Chigunga p/s, olevel Butundwe ss, Alevel Longido high school Arusha na sasa nipo chuo cha Ualimu Monduli Nimewahi kuwa mwenyekiti ukwata miaka Miwili Butundwe,
Mzee wa ukwata Longido ss pia sasa hivi ni Mwenyekiti UKWATA chuo cha Ualimu monduli pia Mwenyekiti UKWATA kanda ya maasai kaskazini , pia
Makamu Mwenyekiti UKWATA mkoa wa Arusha na Manyara
Kwa mapenzi ya mungu tena amenipa somo la kusema na wewe. somo hili Mungu alinipatia katika mazingira ambayo sikutegemea maana nilijiandaa kwenda kuhubiri LOWASA sec kilichotokea notebook niliyokuwa nayo ina masomo mengine ikapotea na baadaye nikamuuliza mungu nifanyeje?
Akanijibu kwa kunipatia somo hili ambalo kweli mara ya kwanza wakaokoka watu 50 na wengine 15 kuponywa na MAPEPO, VIFUNGO VYA MAGONJWA MBALIMBALI
NAOMBA UFUATANE NA MIMI KATIKA SOMO HILI
Mwanzo Mungu wakati anamuumba ADAMU na EVA/HAWA kitu cha kwanza akawbariki na kuwaambia wakazae waongezeke duniani lakini baada ya nyoka kuingia, maana biblia inasema "nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama wote wa mwituni......mwanzo2:1--" huyo nyoka akamdanganya HAWA kuwa akila atafanana na mungu kumbe anabadirisha Baraka kwenda kwenye Laana (mwanzo3:1--6)
 
YALIYOMO:
  • Nini maana ya Baraka?
  • Nini maana ya laana? 
  • Fahamu mambo kumi na mbili ili kuteka Nguvu Mungu
    1. Lazima utambue ni haki yako kubarikiwa
    2. Lazima ukubali kusikiliza sauti ya Mungu ndani mwako na uitendee kazi
    3. Lazima uwe mkweli katika usemi wako na matendo yako
    4. Jitahidi kutambua baraka zako zisiwe kwenye vifungo kisa upendo wa kinafiki
    5. Chunga maneno ya kinywa chako unayoongea kila siku
    6. Tafta kunyenyekea mbele za Mungu na mbele pia za wanadamu
    7. Tambua kuwa baraka zako zimefungiwa kwenye matoleo
    8. Tabia ya uoga : usiwe na tabia ya uoga
    9. Maisha yasiyo mapya na Mungu wako
    10. kutokuwa mtu wa kusoma neno la Mungu na kuomba
    11. Simama katika sala na maombi baada ya kutimiza yale yaliyo hapo juu.
    12. Hakikisha humruhusu tena shetani kucheza na maisha yako tena
Nini maana ya laana? Maana ya laana ni kutengwa na rehema za Mwenyezi Mungu.
Je, unaridhia ndugu yangu kutengwa ... pia maisha unayoishi unauhakika kuwa huna laana yoyote inayokuzunguka na kwa nini maisha yako hivyo kama ulivyo?
naomba ufuatane na mimi katika somo hili maana yawezekana kabisa litakubadilisha na kukufanya ubarikiwe na Baraka za Mungu
Mwanzo Mungu wakati anamuumba Adamu na Hawa aliwabariki akawaambia wazae na kuongezeka duniani lakini baada ya nyoka kuingia ndani yao akabadilisha zikawa laana
Mwanzo3:1-“Basinyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu akawamwabia mwanamke ati hivi ndivyo alivyosema Mungu?----- Nami nitaweka uadui kati yako na huyo Mwanamke------) hivyo kuanzia hapo LAANA zikaingia Duniani na kuanza kutengwa na Rehema za mungu .
Nini maana ya laana?
Maana ya laana ni kutengwa na Rehema za Mungu, Rehema ya Mungu ni sawa na kupata kibali machoni pa Mungu kwaani ndivyo ilivyofanyika kwa Adamu na Hawa baada ya wao kutenda Dhambi walifukuzwa kutoka katika bustani ya Edeni ni Ishara ya kutengwa na Mungu je na wewe umeridhia kutengwa na Rehema za Mungu? Katika maisha yako?

Hebu fuatana nami katika mtiliko wa somo hili ili ujue jinsi ya kuteka hizi baraka za Mungu


FAHAMU YAFUATAYO KATIKAKUTEKA BARAKA/NGUVU ZA MUNGU

1. lazima utambue kuwa kubarikiwa ni haki yako

“Yeremia 29:11 Maana nayjua mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana ni amawzo ya amani wala si ya mabaya kuwapa Tumaini katika siku zenu za usoni”Je nini maana ya Tumaini kwa lugha ya Kiingereza “HOPE” maana halisi ni KUHUISHWA haijalishi utapita wapi ila fahamu kuwa Mungu lazima atakuhuisha na lazima utauona ukuu wake ndivyo Baraka zake zitakavyokujia wewe.walio wengi wanasema anayefaa kubarikiwa ni Mtu flani tu mimi wala sifai hata kidogo kumbe haijalishi wewe ni nani ila mungu anawawazia wote mawazo mema na pia lazima atakupitisha popote pale ila kile anchopenda kukupa lazima atakupatia “Rumi 8:28-Mungu hufanya kazi pamoja na wale wote wampendao katika kuwapatia mema yaani wale walioitwa kwa kusudi lake”. Pia yeye anafanya kazi siku zote na wale wampendao je wewe wampenda Mungu kikweli? Hivyo kama wampenda Mungu kikweli jua anafanya kazi pamoja na wewe katika maisha yako hivyo ni haki yako kutambua kuwa mungu anakuwazia mawazo mema “maana mawazo yangu si mawazo yenu wala njia zangu si njia zenu si njia zangu asema Bwana Isaya 55:8---” Hivyo sio mda wako wa kujikataa mwenyewe kujiona kuwa hufai kumbe unafaa pia hata mawazo yako sio ya Mungu yeye anakuwazia vingine. Hivyo ni haki yako kubarikiwa.

2. lazima usikilize sauti ya mungu ndani mwako na uitendee kazi.

Mara nyingi wengi wetu tumeshindwa kuziona Baraka za Mungu kisa hatusikilizi sauti ya Mungu na wengi tunajitahidi hadi kusoma neon lakini sauti ya Mungu tunashindwa kuskiliza sauti ya Mungu hata kama tunasikiliza mara ngapi tunaifanyia kazi? Angalia mistari hii “kumb28:1-6 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana Mungu wako , kwa bidii kutunza na kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo ndipo Bwana mungu wako juu ya mataifa yote ya Duniani na baraka hizi----” Hivyo usfikiri kuwa Baraka zinakujia ila ni pale tu utakapokaa nakuskiliza sauti ya Mungu na kuifanyia kazi. Nakumbuka mimi na Mchumba wangu tulionywa jambo mbele za Mungu na kilichofuatia tukaacha kulifanya hivyo tulikoswa amani kabisa hadi kufikiria kuwa labda Uchumba wetu sio mpango wa mungu lakini baadaye tukamuliza mungu kwa kulia sana na kufunga kilichotokea hakunyamaza kimya ila yeye alijibu na kutkumbusha alivyotuonya ndipo tukaamua kumsikliza sasa tunaishi vyema bila hata shida yoyote.pamoja na mapito yote kuwa ni magumu lakini Mungu bado anatupigania. Wengi sana wamesahahau kuwa Mungu asiposikilizwa hawezi kutoa Baraka hivyo sikiliza sauti ya Mungu maana maandiko Matakatifu yanasema kuwa “kwa kuwa Mungu hunena mara moja, naam, hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali , katika ndoto katika maono ya usiku usingizi mzito uwajiapo watu katika usingizi kitandani. Ayubu33:14-16” waliowengi kweli hatusikilizi sauti ya mungu na wengi tumekalili kuwa Mungu anasema nasi kwa ndoto pekee wakati ndoto ni matokeo baada ya kuelezwa jambo hilohilo mara mbili lakini bado hujali ndipo anamua kukueleza mara nyingine kwa ndoto angalia mara ngapi Mungu anakushauri kufanya jambo flani harafu unakataa kufanya? harafu nini kinatokea? Wengi pia wangeuliza swali kuwa Mungu anasema nami kwa jinsi gani lakini mimi nakuambia mara nyingi sana anakushauri wewe huelewi hivyo kila ndoto utakayoota leo hakikisha unaiandika harafu ifuatilie uone matokeo yake au kila jambo ambalo Roho Mtakatifu anakushauri kufanya angalia sana yawezekana barakazako zimefungiwa kwako wewe kisa sauti ya Mungu huifanyii kazi mara nyingi unasema “si ndoto tu” kumbuka Mungu ana halisi na kila kitu anachosema na wewe hebu lifanyie kazi harafu utaona faida yake “maana utabarikiwa uingiapo na utokapo ……….”

3. lazima uwe mkweli katika usemi wako na matendo yako:
Na wengi hapa ndio wameshikilia Baraka za Bwana/Mungu maana utamkuta mtu anasema/ Anahubiri lakini yeye mwenyewe halifanyii kazi hivyo ankuwa Muongo na wala sio mkweli “Galatia 5:25 tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho” ni kweli wewe katika huduma yako unaenenda kwa Roho? Mara ngapi umafikia hata kuwambia watu ufuate niyasemayo na usifuate niyatendayo? “Biblia inaniambia jinsi mchungaji alivyo ndivyo kondoo wake walivyo” kama wewe ni kiongozi je unawapeleka wapi wale unaowongoza? Wewe ni kiongozi wa namna gani kama usemi wako hauendani na matendo yako “Biblia inaniambia Tutawatambua kwa matunda yao” matunda yako ni yapi hata wewe unayelia eti huoni Baraka za mungu? je usemi wako siku zote unaashilia katika matendo yako? Maana yale unayoyafanya ndio Mungu anayoyatazama. walio wengi wamevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wakali tena wakuweza kurarua watakatifu wa mungu Bwana yesu asifiwe kwa wingi sana kumbe ndani unaficha maovu ambayo mungu anayaangalia. Jaribu siku zote kuenenda kwa Roho, maana Roho anatabia ya kushuhudia katika kila utakalo kufanya “Zaburi 1:1-6 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki wala hakusimama katika njia ya wakosaji wala hakukaa Barazani pa wenye mizaha” hebu chunguza maongezi yako siku zote ni ya ukweliau yamejaa mizaha na mambo ya ajabu siku zote? Unashangaa wenazako wanabarikiwa harafu wewe hubarikiwi kumbe wewe unakaa na watu wenye mizaha pia na wasio haki ila hakuna lolote unalolifanya juu yao pamoja na kwamba hufanyi lolote baya kumbe shetani anendelea kukunyemelea na kufungia milango ya Baraka. Pia kukutengenezea mzizi wa kwake na hatimaye unaanguka na baadaye ushindwa kusonga mbele na ndipo unakosa baraka za Mungu maana Mungu lazima akutenge naye. Hebu kaa upya na Mungu ili akuangalie vyema Baraka za Mungu zije juu yako, wengi wanasema kwani mbona yesu alisirikiana na wenye dhambi mbona hakutenda dhambi? Lakini kumbuka Yesu alikuwa Mungu pamoja na kuwa alikuja kwa njia ya kibanadamu “biblia inaniambia Haiwezekani kutembea njia moja kama hamjapatana amosi3:7” hivyo antgalia je ukweli wako umanisha nini ? “efeso 4:17-18 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika bwana, tangu sasa msienende kama mataifa yaenendendavyo kwa ubatili wa nia zao……..” Je nia yako sio sawa na watu wa mataifa kama unashirikiana nao pasipo hata kuwasaidia katika kuachana na dhambi hehbu angalia Mungu anpoteza maono yako ambayo amekusudia kukutimizia katika maisha yako je mangapi unahitaji mungu akufanyie? Maana yawezekana maongezi yako hayajakaa sawa kwani siku zote unamsifiya shetani na uhodari wake. “hebu soma hadithi h ii baba mmoja alikuwa anatembea na mkewe gafla wakakutana na mwanamke mbele yao huyo mme wake akamwangalia saana kilichofuatia akanza kumsifia ati huyu dada mzuri saana yaani hebu muangalie matiti, matako, muonekano wake mzuri saana” hivyo baada ya hapo kesi ikaingia hadi nyumbani hatimaye kusababisha kusambaratisha familia” sasa angalia yeye alichokosa ni kumsifia yule mwanamke mwingine hivyo mkewe akachora picha kuwa yawezekana antembea na watu wengine nje ya ndoa kwa nini amsifiye mtu mwingine wakati mie ndiye mkewe? Pamoja na hayo biblia inasema ukimtamani tu mtu tayari umezini naye hivyo ukitamani kazi za shetani kwa kushindwa kusema ukweli ni kuwa karibu na kazi za shetani hata kama huzifanyiila unafunga milango ya Baraka za Mungu kuja juu yako. “Isaya 59:3b Midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya” vitu gani vinatoka kinywani mwako? Viangalie saana yamkini vinapoteza Baraka /amani ndani yako nakupoteza baraka za Mungu.

4. jitahidi kutambua kuwa Baraka zako zimefungiwa kisa upendo wako ni wa kinafiki
Wanadamu wengi saana Mungu ameshindwa kuwabariki kisa Upendo walio nao ni wa kinafiki wengi wanasema wanampenda Mungu lakini ukweli ni kwamba ni waongo kwaani wamechukiana wao kwa kwa wao lakini biblia inasema “1yohana4:20-21 mtu akisema nampenda Mungu naye anamchukia ndugu yake ni muongo kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye anamuona hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumuona” wengi wanasema wanmpenda Mungu hata kama ukiwauliza wanajibu kweli mimi nampenda Mungu lakini ukiwauliza je hakuna ndugu au Rafiki ambaye umekosana naye? Atakuambia yupo! Hivyo ni uongo mkubwa saana haiwezekani hata siku moja ukampenda mungu ambaye hukumuona na bado ukamchukia mwanadamu ambaye unaye kila siku nab ado kumbe umetenda dhambi kubw nab ado unaendelea kuitenda kwani Biblia inaniambia “1yohana3:15 kila amchukiaye ndugu yake ni muaji……..” kumbuka kila muaji hana chake katika uzima wa milele hivyo wewe unatembea kumbe ni muaji angalia mungu asije akakuhukumu maan pamoja na kushindwa kupewa Baraka bado tena wewe ni Muaji. Pia unaomba hupati jibu kumbe kina kitu ambacho unashikilia ndani mwako hutaki hata kukiachilia hivyo Baraka za Mungu haziwezi kupenya hata siku moja na kuja kwako kwa sababu ya hali uliyonayo. Hebu fanya kila uwezalo ili utafte amani na watu wote “Ebrania12:14 Tafteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao” hebu jiulize kama kweli unaamani na watu wote katika maisha yako kusudi ufikilie kuhusu Baraka za Mungu hivyo fanya uwezekano wowote wa kuwa na amani na watu wote wanaokuzunguka kusudi milango ya Baraka ifunguke juu yako. “Efeso 4:2-4 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa Uvumilivu mkichukuliana katika Upendo, na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani .” neno Amani limeng’ang’ania saana maana ndilo linaloruhusu kila jambo kufanyika na fahamu hakuna aliyesabati katika jambo lolote hivyo ni muhimu saana kuachilia chochote ambacho mtu amekukosea kusudi amani iwepo ndani mwako na iweze kuruhusu Baraka za Mungu kuondoa hofu ndani mwako. Hivyo kuwa mvumilivu katika yote unayoyapitia kusudi umuone mungu akikupigania yeye hawezi kukuacha peke yako lazima asimame katika kila jambo unalofanya katika maisha yako. Hivyo tafta kwa bidii zote kuwa na amani na watu wote mungu afungue milango ya baraka juu yako.

5. Tafta sana kunyenyekea mbele za mungu pia kwa wanadamu

Biblia inasema “1petro5:6-7 nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu uliohodari ili awakweze kwa wakati wake” walio wengi wetu tunaona kunyenyekea ni kama kupoteza wakati kama washamba Mungu anapendezwa sana na unyenyekevu wetu tunaouonyesha mbele zake yawezekana hata maombi yako hayapati kibali mbele za mungu kisa kumbehuna tabia ya kunyenyekea mbele za Mungu hebu watu hawa wawili “luka18:9-watu wawili walipanda kwendahekaluni kusali mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Farisayo akasimama akiomba hivimoyoni mwake “Ee Mungu nakushukuru kwa kuwa si mtu kama watu wengine wanyang’anyi, wadhalimu wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga, natoa zaka katika mapato yangu, lakini mtoza Ushuru alisimama mbali wala hakusubutu kuinua macho yake mbinguni hali akijipigapiga kifua akisema Ee Mungu uniwie Radhi mimi mwenye dhambi. Huyu alishuka amehesabiwa haki kuliko Farisayo” kwa nini kwa sababu alijinyenyekesha na kujiona mwenye dhambi hivyo akajikweza. Biblia inatupa majibu ya Shida zetu kwa nini Baraka zako hazionekani? Maana kila ajikwezaye atadhiliwa naye ajiadhiliye atakwezwa/atashushwa. Hivyo angalia moyo wako umejaa nini maana Mungu anaangalia moyo na wala haangalii kama mwanadamu aangalivyo ni dhahiri kuwa kuwa wewe pia Baraka zako hazionekani kisa ni kuwa huna tabia ya kunyenyekea machoni pa Mungu siku zote wewe unajihesabia haki kwa mungu unajikona hakuna ulilomkosa Mungu “Rumi 3:23 wote wametenda dhambi na kupungunkiwa na utukufu wa Mungu” je wewe unajiona uko katika hali gani machoni pa Mungu je ni hali ya kunyenyekea au hali ya kujiinua? Je hujatengwa na mungu? Kwa kufuatwa na laana yamkini zimekutesa sana na kukunyanyasa sana hata huoni mafanikio yako. Hebu fuatana nami tena katika mistari hii “Isaya57:15b Nakaa mimi mahali palipo Patakatifu tena pamoja na yeye aliye na Roho iliyotubu na kunyenyekea ili kuzifufua Roho za wanyenyekevu na kuifufua mioyo yao waliotubu.”hivyo ndugu unayeniskiliza na unayesopma kitabu hiki je wewe upo katika hali ipi? Wewe ni kiongozi popote ulipo yawezekana Mchungaji, Mwinjilisti, Padri Askofu,Mwenyekiti, katibu ngazi yoyote au wewe ni muumini wa kawaida au mtu gani wewe ambaye wafanya mambo yako mwenyewe eti uonekane na watu lakini wewe huna hata wa kunyenyekea kwa Mungu je unategemea nini mbele yako angalia mji wako pamoja na kuwa umeokoka lakini bado huna hata amani katika maisha yako ya ndoa na watoto pia “Je unavyoenda kumuomba mzazi wako kitu chochote unamwambia baba nipe tena mimi nachelewa?”mzazi unaomba kwa nidhamu tena kwa kunyenyekea kwake lakini kwa mungu wako anakaa katika moyo ulionyenyekea. Sasa kwa nini usinyenyekee kwa Mungu aliyekupenda kwanza? Nakushauri uache ushamba kusudi umpe Mungu baba heshima yake tukufu kusudi aachilie baraka juu yako.

6. Chunga maneno ya kinywa chako

Wengi wamefungwa na maneno ya vinywa vyao pia vya wazazi wao bila wao wenyewe kujua kwani wanasonga tu mbele bila hata kutafta ufumbuzi kwa nini baraka zao hazionekani? Fuatana nami katika misitari hii “methali18:21 mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi na wao waupendao watakula matunda yake” maneno gani unatamka maana yawezekana wewe mwenyewe unajikana kuwa mimim siwezi kubarikiwa na hali hii nilishaizoea ni ya kwangu mim lazima niugue kila baada ya majuma mawili hivyo unapanda jambo kama lilivyo halafu linashindikana nabaadaye inakupa shida na majutokwa sababu unatamka neno ambalo ni la mauti hivyo unajiwekea mising ambayo itakupatia matatizo ndani mwako na katika maisha yako pia ndiyoinawezekana kupoteza Baraka zako ambazo Mungu amekuandikia katika maisha yako. Hivyo lolote umelishikilia wewe mwenyewe hivyo angalia sana baraka zako zisize zikapotea kwa sababu ya midomo yako maana ndivyo yenye uzima na mauti. Nakumbuka baada ya kujua haya siku moja tunatania nababu yangu gafla akaniuliza hivi wewe unataka kuzaa watoto wangapi? Nikamwambia kama wanne akakasirika akaniuliza hivi wewe ungekuwepo kama nisingemzaa mama yako? Nikasema babu zamani ni zamani na sasa ni sas kwani mtoto anahitaji kusoma, kuvaa,na matunzo mengine ya msingi. Akasema ngoja wengine tuanze kuwalaani taratibu bora hata usizae kabisa? Mimi nikaingiwa na uchungu nakumbuka nililia sana nikamwambia Mungu juu ya swala hilo na Mungu akafanya jambo babu akajuta kwa nini niliongea lakini cha maajabu Mungu alimuonyesha Babu yangu katika ndoto kuwa mtoto wangu wa kwanza ni wa kike kweli pamoja na hayo majibu yote lakini bado nilishugulikia katika ulimwengu wa Roho mungu akshughulikan na mimi ila bado kilichonikumba ni hofu pamoja na majibu hayo nilitamani hata kuoa mapema kusudi nihakiki kile ambacho mungu alikijibu juu yangu lakini hadi sasa sina hofu wala mashaka maana Mungu anaendelea kunipigania. Hivyo njia mbadala niliyoifanya nikuvunja hayo maneno kwa maombi ya mzigo mungu akafuta hivyo maneno yoyote unayotamka angalia mbele je yatakubariki au yatakulaani? Maana ni bora uchunge kila neno unenalo au unalonenewa na watu wengine, hebu angalia hapa biblia pia inasema jambo mahali hapa “mathayo15:8-9 watuhwa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali naminao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” wengi wenu mnajitahidi sana hata kufundisha lakini kie kilchoko moyoni ni tamaa zenu tu ndio zimejaa na mambo mengine yasiyompa Mungu baba utukufu pia “isaya 57:19 Nayaumba maneno ya vinywa venu amani kwake yeye aliye mbali…..” hivyo mungu anatabia ya kuumba maneno unayoyatamka au uliyotamkiwa na watu wengine angalia sana maana yawezekana Baraka zako zimefunwa kwa sababu ya maneno ya kinywa chako unacho kitakuwa maana kumbuka mungu alisema liwe jua likawa hivyo maneno ya kinywa chako ni kuchunga sana kusudi uruhusu Baraka za mungu zije juu yako.


7. Tambua kuwa Baraka zimefungiwa kwenye matoleo

Kama unakumbuka wana wa Israeli walikuwa wakienda mbele za Mungu na kitu mkononi wanapopeleka jambo lolote na baad ya kujibiwaa walipeleka kitu mkononi kwa ajili ya kumshukuru Mungu hivyo na wewe hebu jitengenezee hayo mazingira maana Mungu lazima aonekane katika Ukuu wake. “Kutoka 23:15b Wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu” wengi wanaona kuwa suala la fedha likiongelewa basi hakuna maana yoyote lakini kuna siri kubwa sana katika utoaji na wengi hapa hawapajui nahapa kinahitajika kabisa ujue umuhimu wa matoleo katika maisha yako yawezekana kabisa Mungu anashindwa kukubariki kwa sababu yaw ewe kutokuwa na moyo wa utowaji maana kama wewe huwezi kutoa unategemea upokee kwa nani? Biblia inasema ni bora kutoa kuliko kupokea. Kumbuka Mungu sio maskini hata siku moja ila anchoangalia kwetu ni utii wako yeye anaweza hata akakubariki hata kama hujampatia kitu chochote kile ila anachoangalia kutoka kwetu tunamweshimu kiasi gani kwa kile anachotupatia. Hebu angalia tena” kumbu29:29 Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi sisi na watoto wetu milele ili tufanye maneno yote ya sheria hii.” Pale ambapo wengi wanashindwa kuelewa maana mambo mengi sana yamefichwa na machache ndiyo yamefunuliwa na ndiyo yetu hivyo kama unataka kuruhusu kufungua jambo lolote hakikisha unafanya maana yawezekana hata Baraka zako zimefungiwa hapo pia katika ulimwengu wa Roho. Ambao umeficha mambo mengi sana hivyo fanya hima uweze kuchukua kile kilichoko kwenye ulimwengu wa Roho. “Mwanzo15:8-13 Akasema Ee Bwana Mungu nitapataje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwambia unipatie ndama….” Kipindi kile walipewa kila jambo kwa maagizo maalumu pale walipotoa kitu alichowaagiza Mungu hebu ndugu jiulize mara ngapi umeomba ubarikiwe lakini unashangaa hupati Baraka? Sababu kubwa ni kuwa hutaki kutoa maana Mungu anapenda sana umtolee hasa moyo wako kusudi uwe sadaka safi mbele zake kusudi Akubariki. Kumbuka Esau aliambiwa na baba yake Isack kuwa amwandalie chakula kusudi aweze kumbariki. Hivyo fahamu kuwa Baraka za Mungu pia zitegemea uende na kitu mkononi ili aweze Kukubariki simanishi kuwa labda lazima uwe na kitu halisi lakini pia Moyo wako ni sadaka tosha kabisa machoni pa Mungu. Nakushauri umutolee Mungu sadaka ya kila jambo ambalo yeye anatamani kufanya juu yako lakini pia pamoja na wewe kumbuka kumshukuru kila wakati kwa chochote ulichonacho.


8. Usiwe na tabia ya uoga tena katika kuteka Baraka zako
Mungu hakutuumba na Roho ya uoga/hofu maana walio wengi wana Roho ya uoga na hata kama anaona Baraka za Mungu zipo juu yake kwa hiyo zile Baraka zinakuwepo ila unakuwa umetengwa na Mungu hivyo unashindwa kupoekea chochote kutoka kwa Mungu aliyehai hebu angalia hapa “Ebrania10:38b mwenye haki yangu ataishi kwa imani naye akisitasita Roho yangu haina Furaha naye” hebu chukua neon “Haina Furaha naye” maana yake ni kuwa Mungu amekutenga kabisa naye ndiyo maana hata hana Furaha na wewe hivi chukulia motto anayefurahiwa nyumbani yukoje ? mara nyingi ndiye husikilizwa tu kiliko wengine wote. Hivyo kama unapenda upendeleo basi fanya uhusiano wako na Mungu usiwe na Hofu na wala mungu hatacha kukupenda. Hebu mwangalie Joshua kwa nini Mungu alirudia sana haya maneno? Akaambiwa usiogope kwa nini maana Mungu aalijua hofu ni Dhambi na inafunga Mirango ya Mungu kuwasiliana na wewe maana tayari angekuwa ametengwa na Mungu hivyo alijua kama angeogopa tu basi asingeweza kufanya kazi ya Mungu aliyotamani mungu aifanye kwa wana wa Israel Yoshua 1: 9 "je si mimi niliyekuamuru? uwe Hodari na moyo wa ushujaa, usiogope wala usifadhaike kwa kuwa BWANA, Mungu wako yu pamoja nawe kila uendako" hebu na wewe anza kuchukua hatua ya kutoogopa katika maisha yako mafanikio yako yanakuja usikate tamaa yoshua aliambiwa na mungu kuwa Mungu yuko pamoja na yeye kila aendako hivyo acha uoga mtoto wa Mungu baraka za munu zaweza kupita mbali na wewe maana kumbuka hofu inaleta majuto na mateso katika maisha yako hivyo kimbilia kwa Yesu kusudi aondoe uoga wote mbele zako maana Mungu anasema hawezi kukusahau maana amekuchora katika vitanga vya mikono yake " Isaya 49:14-16 ............Naam hawa waweza kusahaulakini mimi sitakusahau wewe tazama nimekuchora kwenye vitanga vya mikono yangu" hivyo huna haja ya kuogopa na wala hawezi kukusahau katika hali yoyote uliyonayo ambayo inakusumbua na wala usiwe na wakti wa kuogopa wala kuwa na Hofu amini tu maana yeye atafanya kwani si mwanadamu hata aseme uongo "Hesabu 23:19 Mungu si mtu hata aseme uongo wala si mwanadamu ajute, iwapo amenena hatalifikiliza? iwapo amesema hatalitenda? hivyo acha ushamba wa wokovu unaokoka lakini bado uanendelea na dhambi ndio maana unakuwa nawasiwasi na mashaka kumbka mungu yupo atakusaidia ansema yeye hakumbki tena dhambi zako. wewe kana umetubu kutoka ndani ya moyo basi anza kujisamehe mwenyewe wala usijihukumu. "Isaya 43:18,25 msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani, mimi nami mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala sitazikumbuka dhambi zako" mungu mwenyewe ansema hawezi kukumbuka dhambi zako sasa wewe unazikumbuka za nini kiasi ambapo umetubu unahukumiwa na nini? tena mtoto wa Munu kwani tabia ya mungu ni kusamehe na kusaha sasa ila shetani siku zote yeye ni kukumbusha kusudi ujione mwenye makosa siku zote hivyo usimuache mungu kwa kukumbushwa yale uliyoyafanyan hayawezi kukuondoa katika upendo wa Mungu hivyo songa mbele usimwache Mungu.


9. Anza maisha mapya na mungu
maisha mapya na yesu yanaanzia ndani ya moyo kumbuka toka mwanzo tumeongelea Barka hivyo vinaendana sana na kukaa katika hali ya utakatifu ili uwepo wake Mungu auachilie mbele zako na usije ukawa katika wakati mgumu wa kushindwa kuwa na uhusiano mzuri na mungu biblia inasema "Rumi 11:16 -- tena malimbuko yakiwa matakatifu kadharika na donge lote na shina likiwa takatifu matawi nayo kadhalika" hivyo fahamu maisha yako kuwa safi yana mruhusu mungu kushusha baraka zake kama malimbuko yakiwa mataktifu na dongenalo lote hivyo litakuwa takatifu kama Roho, mwili na nafsi vikiwa safi kumbuka mungu lazima achirie nguvu zake sana kwako na kukupa baraka na hatimaye kupewa uhuru wa kutembea katika nuru yake mungu aliye hai, na kumbuka mungu akiwa upande wako lazima mambo mengi sana yataenda sawa hata kama ukipokea jambo lolote ambalo ni gumu kwako lazima mungu akupatie uwezo wa kupambana nalo hivyo acha kuwa na maisha yasio ya wokovu tembea na baraka za mungu katika kufanya maisha yako siku zote yawe na amni tele. kwani maisha mapya na yesu ni maihsa ambayo yana kila utukufu utokanao na mungu aliye hai hivyo anza kutembea na mungu siku zote za maisha yako yeye atakupatia jawabu la maisha yako. ninavyoandika kitabu hiki mungu alinifundisha kitu kwani nilikuwa kwenye majuto makubwa baada ya kumtenda mungu dhambi kwa kusukumwa na tamaa zangu mwenyewe kwani mungu aliniambia jambo halafu nikapuuza hatimaye majuto mfululizo ndani mwangu ambayo yalinikosesha amani skiuona hata haja ya mimi kuishi katika dunia hii lakini mungu alivyo wa huruma alinisamehe nayo yote sisemi kwamba siwezi kutenda dhambi bali naishi katika maisha ya toba siku zote hivyo mungu ni mkuu anaangali mwisho haangalii mwanzo wa jambo angalia wewe uko katika hatua gani hata kama umemtenda mungu dgambi ya namna gani hakuna kitu ambacho atashindwa kukusamehe hebu mwambie mungu aachilie ndani mwako kuysudi akusamehe "Isaya 1:18-19 Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama damu zitakuwa nyeupe kama sufu" hivyo mungu anaweza kukusamehe nayo yote hivyo kila ambacho unakiona ukinashikilia moyo wako lazima ukubali kuwa mpya katika usemi wako matendo yako pia maana yawezekana ukawa mpya katika maneno lakini matendo ukawa mbali na mungu, Anza mambo mapya na Yesu kristo. Paulo alisema nakaza mwendo nifikie mede ya zawadi ya ushindi, sio kuwa nimesimama la hasha, hivyo kuna magumu aliyoyapitia " akasema nikiuangalia uzuri ulio katika kristo Yesu nayahesabu yote kuwa kama mavi, hata wewe waweza kuhesabu mazuri yote ambayo unauhakika kabsa kuwa unafanya bila msaada wa mungu baba kuwa kama mavi angalia uzuri ulio katika kristo kusudi akukukomboe kwani unajua nini juu ya mavi? sijua kama ukiambiwa shika kinyesi au mavi kama unaweza hata kuyashika mkononi mwako hebu amua kuanza maisha mapya na yesu kusudi akubadilishe uwe kiumbe kipya


10. Simama katika neno la mungu/jitahidi kusoma neno


kumbuka kati ya mising yote ya kusimama na kuteka Baraka za munguni wewe kusimama katika neno la Mungu maana Biblia inasema "zaburi 119:105 neno la mungu ni taa ya miguu yangu" kumbuka kama ni kwenye giza sina uhakika kama unaweza kutembea kwa amani kwani lazim utakuwa muoga na huo uoga utakufanya ushindwe kuona hata mbele unakoelekea kwani ni lazima uone ndipo uweze kufanya jambo lolote kwa nguvu zote hivyo kama huwezi kuona huwezi kusonga mbele tumia neno la mungu kusudi liwe taa ya miguu yako kusudi uweze kutembea na uweze kuteka baraka za mungu. hivyo mising ya matoleo, Ibaada, utii vyote vinatokana na neno la mungu hivyo huwezi kutembea kwa hatua yoyote bila neno la mungu kwani mungu ni kiongozi kupitia katika neno lake. lakini huwezi kupokea Baraka zako au hata maombi yako usiposimama katika neno la Mungu "1korintho7:5" pia biblia inasema "Yohana15:7 ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani mwenu, ombeni neno lolote nanyi mtatendewa" kumbe mambo mengi sana ya kwako yamefungiwa katika ulimwengu wa roho kisa wewe husomi neno maana kumbuka bila neno la mungu ndani mwako huwezi kujua hata jinsi ya kushinda dhambi pia ukishindwa na dhambi fahamu Mungu amekutenga na kama umetngwa tayari maisha yako hatarini sana maana barka zako zote zimefungiwa lakini ukiwa na misingi ya neno basi kila litakalokuja kwako utajua jinsi gani uweze kushinda maanadhambi yoyote inaziba milango ya baraka na mafanikio mbele zako hivyo jitahidi siku zote usome neno la mungu kama wewe nimwanafunzi jitahidi kuweka kwenye ratiba yako hivyo uwe angalau dakika chache kutafakari neno la mungu itakusaidia sana kuwa karibu na mungu katika nyakati zote kwa siku nzima. Pia kama wewe ni mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara anza n aneno asubuhi na pia usiku angalau uwe karibu na mungu aliye hai maana una heri wewe unayetafakari neno la mungu usiku na mchana jani lake halitanyauka kamwe na kila alitendalo litafanikiwa. kumbuka pia Yesu mwenyewe alikuwa na neno kiasi ambacho kilimsaidia kumshinda shetani wakati anajaribiwa kwenye siku arobaini za kufunga alisema "imeandikwa " biblia inasema wakamshinda ibilisi kwa ushuda wa neno la mungu na wewe siku zote jitahidi sana kusoma neno lake kwani sio lazima sana kila sehemu unakoenda uende na biblia lakini waweza kuwa na neno tu ndani likakusaidia hivyo jitahidi siku zote kuwa na neno ndani mwako ili uweze kupokea sawasawa na mapenzi ya mungu sawasawa na mahitaji yako. kwani mungu ansifa yake ya pekee sana kwanza hawezi kusema uongo pia yeye ni mkweli tu anasema "naliangalia neno langu nikapate kulitimiza" hivyo anchoangalia ni neno aweze kutimiza ndani mwako kulingana na mahitaji yako ya kila siku unayomuomba. hivyo neno ni ufunguo wa baraka za mungu aliye hai katika kukupatia baraka zako ambazo zimefichwa kwani neno ni chanzo cha mafanikio yote ndani mwako. mungu anatmani kila mmoja wetu ampatie baraka zake ila jinsi ambavyo umesimama anshindwa kukupatia hebu fanya biblia iwe ndio taa ya miguu yako uone kama mungu hatakufiunguli milango ya baraka kwako? nakutakia maisha mema na yaliyojaa baraka za mungu katika kumjua mungu na kumtumia kusudi kucheka kwako kuwe ni furaha ya kweli ndani mwako na wala usicheke tukwa kuwa wewe umeokoka halafu ndani mwako unamia kumbe hata huoni uthamani wa wokovu wako.


FAIDA ZA KUKAA KATIKA NENO LOA MUNGU
Lakini naomba ufuatane nami kusudi ufahamu tabia na faida za neno la mungu.
a) Faida za kukaa katika neno la mungu
  • kuteka baraka (kumb28:1-4, luka 11:28)
    mlango wa majibu ya mungu(hesabu 11:23, yohana 15:7)
  • kinga ya dhambi (zabri 119:11, 2kor 3:2-3
  • kiongozi wa maisha (zabri119:105, 1samweli 3:1)
  • ulinzi (yohana 8:31,47, efeso6:17)

a) Faida za kukaa katika neno la mungu
1. kuteka baraka
luka 11:28 lakini yeye alisema afadhali " heri wao walisikio neno la mungu na kulishika " maana ya heri ni Baraka hivyo una baraka wewe unayelihika neno la mungu na kufuaata pia kumbu 28; 1-4" na baraka hizi zitakapokujilia na kukupata usikiapo sauti ya bwana mungu wako" hivyo mungu anaweza kukbariki kama utasikia sauti yake na kuifuata na hapa anamaanisha maandiko yake matakatifu usiache baraka za mungu zikupite mtoto wa mungu
2. Mlango wa majibu ya mungu
"Hesabu 11:23 Bwana akamwambia Musa je mkono wa bwana umepungua urefu wake? sasa utaona neno langu litatimizwa kwako au sivyo" maana alitumia maneno lakini wana wa Israel hawakusikia maana walishindwa kufanya kulingana na neno la Mungu akasema na Musa. hivyo pia kwako wewe unayesoma kitabu hiki je maangapi huyapokei maana mlango uumefungwa kwani pia umeambiwa ni taa ya miguu yako je utapitaje kupata mahitaji yako wakati mbele kuna giza kwani milango imefungwa huweziona wapi mwanga unatoka wa kumulika njia zako? "yohana 15:7 Maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lolote nanyi mtapewa" hivyo huu ni mlango wa majibu ya Mungu kwani bila neno la mungu atakujibu vipi maombi yako? weka neno ndani kusudi uweze kupokea majibu ya Mungu wako kwa kila kitu unachomuomba
3. Kinga ya dhambi
"zaburi 119:11 moyoni mwako nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi" hivyo neno la mungu ndilo chanzo chako wewe kutokutenda dhambi. kumbe kama hauna neno ndani mwako uwezekano wa kutenda dhambi upo mkubwa sana hivyo kama ndani mwako kama una neno la mungu hivyo jua una mlinzi imara ambaye atakuweka huru kila siku juu ya adui ibilisi shetani. "2korintho 3:2-3 ninyi ndinyi barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu inajulikana na kusomwa na watu wote" kupitia neno la mungu watu wataona matunda ambayo unazaa maana unasomeka hivyo lazima dhambi kwako itakuwa mwiko huwezi kukaa nayo karibu au pia utaikikmbia kama ikija karibu na wewe maana unaye neno ambaye ni mlinzi wa kweli
4. Kiongozi wa maisha
"zaburi 119:105 neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia zangu" neno la mungu ndie kiongozi wa maisha yako ya kila siku maana bila neno la mungu hauna mwanga wowote wa njia zako hivyo lazima uwe na neno ambalo litatumika kama kiongozi hata kama wazazi ya ani baba na mama yako wakikukataa bado Mungu kupitia neno lake atakuwa mzazi wako. nakumbuka mimi Baba yangu mwaka 1999 alinikataa na kusema siye mwanae nikashindwa shule yaani form One lakini nilimung'ang'ania mungu ambaye ndiye akawa mzazi wangu hivyo akanipigania na mwaka wa 2009 nilimaaliza masomo ya STASHAHADA ya UALIMU kwa sababu YESU amekuwa kiongozi wa maisha yangu hata mimi mwenyewe nashangaa kwani Yesu Kristo mwenyewe amekuwa akinitia Nguvu.  nimekuwa kazini kwa mda wa mwaka mzima ila sikuacha kazi ya Mungu kupitia neno lake leo ninapoandika kitabu hiki nipo CHUO KIKUU CHA RUAHA NIKISOMA DEGREE YA COMPUTER SCIENCE(software--Engineering)  lakini ni kupitia katika neno lake amekuwa kiongozi na mzazi wangu hata leo hajaniacha kamwe sitaogopa jambo lolote ninaye kiongozi asiyetetereka. hebu muone mtoto mwingine wa hana mke wa elkana akimwomba Mungu akampa mtoto kupitia neno la Mungu Samweli akakua katika himaya ya Eli "1samweli 3:31 Basi samweli (mtoto) akamtumikia Bwana mbele ya eli na neno la Mungu lilikuwa adimu siku zile" Mungu alikuwa kiongozi kupitia maneno yake mwenyewe na akawa mtumishi mwema machoni pa Mungu hivyo hata wewe mruhusu mungu kupitia katika neno lake awe kiongozi wa maisha yako hutaona upweke hata kama utapitia wakati ukoje?
5. Ulinzi
"Yohana 8:31 ninyi mkikaa katika neno langu mmekuwa wanfunzi wangu kweli kweli" kama haukai katika neno la mungu fahamu wewe sio mwanafunzi wa yesu kweli kweli. maana yeye anakuwekea ulinzi kama akiona neno ndani mwako kwa sababu anakikit cha kujivunia ndani mwako ambao ni msingi wa neno lake katika maishasha yako mtu wa mungu "yohana 8:47 yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya mungu hivyo ninyi hamskii kwa sababu si wa Mungu" je Mungu anakuambia kitu gani au hata huelewi kwa sabau neno la Mungu halimo ndani mwako maana neno ndiye Mlinzi wa maisha yako yote hapa duniani maana mungu hawezi kukuhesabu kama mwanae kama hauna neno lake ndani mwako "efeso 6:17 tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la mungu"kwa hiyo kama hauna neno hivyo hauna ulinzi wowote maana angalia neno ni chapeo ya wokovu pia bado ni upanga wa Roho hivyo kuwa na uhakika wa ukristo wako bado unaweza kufanya yakupendezayo kwa kusimama katika neno kwani neno litakulinda zidi ya malaya hutakaa uwawaze katika maisha yako kwa sababu una ulinzi ambao ni neno la mungu tena kwa ujumla huwezi huwezi kushinda kwa namna yoyote ile kama hauna neno kumbuka Mtumishi wa Mungu Daudi na udogo wake alimwmbia maneno hya Goliati "1samweli 17:45 wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi ya Israel uliowatukana" kwa sababu mtumishi wa Mungu Daudi alitumia neno la Mungu ambalo ni ulinzi ndio maana aliongea kwa ujasiri akaweza kushinda, pia Sauli alikuwa na hofu lakini Mungu alitaka kuzizihirisha nguvu zake kupitia neno lake. kwa hiyo ndugu yangu kama hauna neno jua huwezi kushinda uovu wa aina yoyote ile maana lazima usimame katika neno ndipo uweze kushinda kila aina ya majaribu mbele yako kwa upeo wngu nakuona kabsa hauna walinzi wowote wakukusidia hivyo ukivamiwa na shetani huwezi kusimama na kushindana naye. Tafta ulinzi nugu yangu kusudi unusuru Roho yako zidi ya maisha haya uliyonayo kusudi ukutane na nguvu za mungu.

b) SIFA ZA NENO LA MUNGU NDANI MWAKO
  • movement (kusogea) (Zaburi 119:28)
  • reproduction(kuzaa matunda) (1petro 1:23)
  • excretion (kutoa uchafu) (zabr 119:133)
  • growth (kukua) (1Petro 2:2)
  • respiration( kupumua) (galatia2:20)
  • response (kuhisi) (mathayo 4:4-) 
b) Sifa za neno la Mungu ndani mwako
kwamba biblia inasema tutawatambua watu kwa matunda yao hivyo tuoni mahali hapa tutaona tabia ya neno ndani mwako au neno lifanya kazi gani kwako mtu wa mungu? "ebrania 4:12 maana NENO la mungu li hai, tena nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafasi na mRoho, na viungo na mafuta yalyomo ndani yake tena li jepesi kuyatambua makusudi ya moyo" hivyo neno lina tabia sawa kabsa na za kiumbe hai hivyo kama neno la Mungu lazima sifa sifuatazo zikosekane kwako kwani wewe unatembea huku umekufa siku zote mtoto wa mungu
1. Movement kusogea /kutembea