Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Maarufu Tanzania
Mungu ameibariki
Tanzania Kwa Kila aina ya Baraka za Mwilini na rohoni. Leo na wiki
chache zijazo nitakujuza Watumishi 25 ambao ukiwataja kwenye mikoa zaidi
ya Kumi hapa Tanzania yamikini wameshasikika na unaweza pata comments
toka kwa waumini wao. Kuna Makanisa ambayo pengine yamesikika zaidi
kuliko kuliko majina ya watumishi hao ama kuna watumishi wamesikika
zaidi kuliko hata Makanisa wanayochunga.
Kuna Watumishi
ambao wamekuwa maarufu sababu ya huduma zao kwa Ujumla, Sababu utajiri
wao, sababu za huduma zao kwa wanafunzi ama kwa program zao za mahali
pamoja.
lengo la Makala
haya si kutafuta nani yuko Juu zaidi ya mwingine ila kutoa taarifa kwa
umma na kuwatia moyo watumishi hawa kuwa kazi yao imevuka mipaka ya
mikoa na nchi.
Yawezekana vigezo vyako sio vugezo vyangu katika kuwasilisha.
Apostle Maboya(Ni
kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo
kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo
la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiX_0uTOrPOiFxMwozRxohSYe64lQAn4EKkCYlUd115ZiUsCnH073YbmIGeAa6Mhij7BFwpLq5x8F7dqegoPyVsiFCDc8GcQxN04uoXONuYCuVbV41VWQPJhmT2IHvGNEAvaRSgC8iNz3U/s320/222814399_19dab0166a_m.jpg)
Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini
Mwalimu Christopher
Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye
huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na
makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya
New Life Crusade/ New Life in Christ.
Mchungaji
Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina
lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka
mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha
siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa
miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata
kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na
amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni
muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.
Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.
Mtume Veron
Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa
kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa
Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa
Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.
Askofu Moses Kulola
wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi
waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za
leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi
mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya
mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu
wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko
yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila
kona ya Tanzania
Nabii GeorDavie wa
GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa
kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.
Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.
Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa
kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM)
na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu
mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna
lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste
Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.ni hao kwa leo tutaendelea kukujuza zaidi endelea kufuatilia
No comments:
Post a Comment
YOUR WORMY WELCOME TO SAY ANYTHING TO ME IN MY WEBSITE