Katika
Maisha yetu ya kila siku mara nyingi tunajikuta katika mazingira
yanayotulazimu kufanya maamuzi magumu au kuchagua kitu katikati ya vitu
vingi ambavyo vinatuchanganya akili. Wengi wetu kwa ugumu huu
wamejikuta wakifanya maamuzi mabovu na kuchagua chaguzi mbovu ambazo ama
ziliwapa hasara au ziliharibu kabisa muelekeo au mustakabali wa maisha
yao. Ndio maana wenzetu wa magharibi (Ulaya) wanamsemo usemao “Life is
how you make Decisions” Maisha ni vile unavyofanya maamuzi.
Tunavyofanya
maamuzi fulani, hususani katika kuchagua vitu kati ya vingi
hatumaanishi vyote au vile vingine ni vibaya bali hatuwezi kuvichagua
vyote kwa wakati mmoja na hivyo tunalazimika kufanya maamuzi ya kuanza
na kimoja na kumalizia na vingine.
Mfano:
Msichana aliyeomba kazi na wakati huo huo ameomba nafasi ya chuo na
pia yuko katika mahusiano na mchumba wake anayehitaji waowane. Hali
hii inamfanya msichana huyu kuwa katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi
nini afanye kwanza na nini kifuate badae.
Daima
huwezi kufanya vitu vyote vilivyo mbele yako, huwezi kuchukua kila
fursa inayokujia lazima uwe na uwezo wa kufanya maamuzi yaliyo bora.
Maamuzi haya yatachangia sana katika kufika mwisho wenye ushindi au
katika kufikia mwisho wenye majuto na machozi.
Katika
makala hii nitajaribu kukupa mbinu tofautitofauti ambazo zitakuwezesha
kufanya maamuzi yako kwa haraka, kwa ubora na bado ukawa katika uwezo
wa kuyasimamia maamuzi hayo.
1. Angalia na zitafute fursa mbalimbali
- Jambo la kwanza ni uwezo wa kuzidaka fursa pale zinapojitokeza
- Jambo la pili ni uwezo wa kuzitengeneza fursa wewe mwenyewe
Katika
jambo la kwanza, la uwezo wa kuzidaka fursa, namaanisha kuwa, baada ya
kueleza au kutangaza kwa marafiki na kupitia njia mbalimbali kuwa
unataka au kutafuta kitu au kazi fulani, haupaswi kukaa tu kimya na
kulala, fursa zaweza kwanza kuja kupitia marafiki zako, wafanyakazi
wenzako, au kupitia matangazo uliyoyafanya maeneo mbalimbali, sasa
hapa haustahili kulala bali kuzidaka na kuzifanyia kazi fursa hizo.
Katika
jambo la pili, namaanisha uwezo wa kuzitengeneza fursa wewe mwenyewe.
Kama kweli unahitaji kitu lazima ufungue macho kutafuta nini tatizo la
jamii inayokuzunguka, wakati wote tatizo au hitaji la jamii laweza
kugeuzwa kuwa fursa. Mfano, kama sehemu ni kame na maji ni tatizo
jitahidi kuchimba kisima, kwa kutatua tatizo lililosumbua jamii umepata
fursa ya kufanya biashara. Usikae tu na kusubiri fursa zijihudhurishe
miguuni pako zenyewe. “run for them”.
Njia zote hizi mbili hazinabudi kutiliwa mkazo na kila mtu.
a) Jizindue wewe mwenyewe
Mara
nyingi tunasikia neno uzinduzi. Hapa naamanisha tendo la kuchukua na
kuuendea mkondo uliouchagua ukutoe kimaisha. Anza kupiga mbio kwenye
njia unayoona itakutoa. (fanya uzinduzi wako mwenyewe bila kusubiri
ufanyiwe). Ili kuweza kujizindua pasipo kuchelewa, lazima kufuata
ushauri ufuatao.
· Jiulize Swali “Ni nini?”.
Kila wakati jiulize ni nini ninachotaka kukifanya na katika hiki ninachotaka kukifanya, ni nini ninachotaka kukipata?
Unaporuhusu
akili yako kufahamu ni nini unachotaka kukipata, unauruhusu mwili na
nafsi yako kujitia nguvu tayari kwa kukiendea hicho kitu.
Faida
nyingine ya kujiuliza ni nini ninachokitaka ni kukupa picha ya ukubwa
au umuhimu wa kile unachokitaka ili uweze kuandaa kila kinachowezekana
kama vile rasilimali vitu au rasilimali watu, au rasilimali fedha ili
kuhakikisha unakipata kile unachokihitaji.
· Uwe
tayari kupata hasara! (be a risk taker) Kama wewe ni mwoga wa
kushindwa au mwoga wa kupata hasara kamwe hutoweza kujizindua kwa
haraka. Kwa ajili hii lazima ujue jinsi ya kushuhulikia hizo hofu
zako. Usiogope kupata hasara katika chochote ufanyacho maana kupitia
hasara tunajifunza mbinu bora zaidi za kuitafuta faida kubwa.
b) Yatumie vema na kwa ufanisi maamuzi yako.
Ili
uweze kuyatumia vema na kwa ufanisi maamuzi yako, tu utumie mfano huu.
Jifikirie umebeba glasi tupu mkononi mwako, waweza kuijaza glasi hiyo
kwa majuto na lawama za uliyowahi kuyafanya au waweza kuijaza kwa
yale uliyojifunza huko nyuma kwaajili ya kesho yako. Kama utabaki
kujuta na kulaumu yaliyopita au uliko sasa hutofaidika chochote kiujuzi
kwa ajili ya kesho yako. Lakini kama utafanya kila unalokutana nalo
kuwa ni somo utapata ujuzi tele kwa kesho yako.
Pinga tabia ya kulaumu na kujutia maamuzi yako kwa kuzingatia ukweli kwamba
· Mambo mengi hutokea au hutegemea na mitazamo uliyonayo.
Maamuzi
mengi tufanyayo hutegemea na mitazamo tuliyonayo maishani. Kama
mtazamo wako ni wakujutia kila kitu au kulaumu wengine, basi utalaumu na
kujutia kila utakachowahi kukifanya, mfano; utajutia na kulaumu kozi
unayosoma, kazi unayofanya, biashara unayofanya, mke au mume mliyeoana
nae, watoto uliowazaa nk.
· Maamuzi
ufanyayo yanategemeana sana na mfumo wako wa maisha. maamuzi yako
maishani hutegemea sana na kile unachokiamini. Kile ulichotayari
kukisimamia na kukitetea, hutegemea sana uasili wa maadili yako, kupitia
hivi vitu tunapata maamuzi mabaya au maamuzi mazuri. Mfano; maamuzi
ya mtu mwenye maaadili ya kidini ni tofauti na maamuzi ya yule asiye na
dini.
2. Jifunze kufanya uamuzi
Jitahidi kuweka misimamo na malengo sahihi katika maisha yako.
Jaribu kuwa na msimamo fulani badala tu ya kuelea elea tu hewani ukisubiri wengine wakusaidie kuamua.
Jitahidi kuyatetea na kujasimamia maamuzi uiliyofanya.
Yathibitishe maamuzi yako kabla hujaamua kuyaacha na kufuata maamuzi mengine.
Anthony
Robbins – Mwandishi na mhamasishaji maarufu ametoa maana halisi ya neno
maamuzi (Decision). Anasema neno hili limechimbuka toka maneno mawili
ya kilatini “de”- ikimaanisha “from” (kutoka) na “caedere”-ikimaanisha
“to cut” (kukata) kwa ujumla wake inamaanisha wakati tunapofanya
uamuzi wowote tunazikatilia mbali fursa nyingine zozote na kuchukua ile
tu tuliyoiamua. Mfano mzuri unapoamua kumuoa binti fulani, hatakama
uliwapenda wengi unalazimika kuwasahau wengine wote.
Pasipo kufanya jambo hili utakuwa hufanyi uamuzi
bali ni matamanio tu. Fahamu dhahiri kuwa uamuzi wakweli unamaanisha
kujitoa, kujifunga katika lile uliloliamua. Na sio suala la kubahatisha
tu.
Unafanyaje Pale unapojikuta umefanya maamuzi yanayosababisha tatizio
Sio
wakati wote maamuzi tunayoyafanya yanatufikisha pazuri au kutuletea
matokeo mazuri. Marangnyingine unajikuta mara tu ulipoamua kujizindua
mwenyewe, maamuzi hayo yanakutupa kwenye hasara au majuto. Unafanyaje
hili linapotokea?
Ushauri!
· Amini ujasiri wako
· Nikosa
kubwa sana kujikosoa na kujisuta na kuusuta ujarisi uliokuwanao mara tu
baada ya kujiona umefanya kosa. Fahamu kwa wakati wowote unapofanya
jambo la kijasiri kuna mambo mawili, labda upate matokeo mazuri au upate
matokeo mabaya. Lakini, kupata matokeo mabaya kwa sasa hakubadili
ukweli kwamba kile kilichofanyika kilifanywa kwa ujasiri.
Ruhusu
kushindwa kwako kuwe kitu cha kukukumbusha kwamba yote hayo
unayoyapitia ni matokeo ya ujasiri wako. Kama usingekuwa jasiri
usingejaribu.
· Jiambie mwenyewe kwamba bado utaendelea kuishi.
Usalama
wa kweli hautokani na kule kupata vile tunavyovihitaji, bali katika
uwezo wa kustahimili zile nyakati tunazojikuta tukizipitia.
Kama unaimani basi amini kwamba bado Mungu yuko na wewe.
Wawezajikuta unapata kazi kubwa na yenye uhakika sana na ukajikuta unaitegemea hiyo na kesho yake kampuni inafungwa au kufa.
· Chukua masomo yaliyo muhimu katika changamoto za maisha
Katika
kila hali tunayopitia hakuna cha kuacha kisichokuwa shule nzuri itakayo
kusaidia kesho. Jifunze kuyatazama mapito magumu kama darasa la
kujifunza kustahimili kesho, yamkini isiwe shule itakayokusaidia wewe,
lakini kwa kuyajua hayo uliyiojifunza utawakwamua wengi watakao kwama
katika tope linalo fanana na lakwako kesho.
Katika
mapito haya Jifunze ni nini chakukirudia tena kesho na ni nini kisicho
faa kurudiwa tena. Sehemu ya Maisha yenye mafanikio ni pamoja na uwezo
wa kujifunza na kukua kukoka uzoefu hadi uzoefu.
1xbet | 1xbet | Bet with a Bonus - RMC | Riders Casino
ReplyDelete1XBet 1xbet app allows you https://febcasino.com/review/merit-casino/ to febcasino.com bet on any favourite horse races or any other sporting event. ✓ Get 스포츠 토토 사이트 up to £300 출장안마 + 200 Free Spins No Deposit