Utafiti
uliofanywa katika maeneo mengi katika nchi zilizo endelea na
zinazoendelea unaonyesha kuwa watu wengi bado wanahitaji kiwango kikubwa
cha uwezo wa kujisaidia wenyewe. Hata
katika nchi kama marekani ambayo teknolojia ni kubwa lakini watu pia
wanakiu kubwa ya jinsi ya kujua kujisaidia wenyewe katika baadhi ya
mambo yanayowasibu kimwili, kihisia na maisha kwa ujumla
Wachunguzi
wakubwa wa maswala ya kisaikolijia Richard na Tony Robbins wanaafiki
kwamba yawezekana kabisa tukarekebisha na kuweka sawa vile visivyokaa
sawa katika miili yetu au akili zetu pasipo kutegemea msaada wa daktari
au mshauri.
Watu
wengi ulimwenguni wanapata msada wa ujuzi huu kupitia kuenea kwa
mtandao wa intanet na vitabu vya ujuzi huu vilivyo vingi sana (self help
books).
Takwimu
zinaonyesha wamarekani walitumia zaidi ya dola 563 milioni kwa manunuzi
ya vitabu vya ujuzi wa kujisaidia mwenyewe, na pia zaidi ya tovuti
12000 za masuala ya afya ya akili “mental health” hutumika nchini
marekani. Yote hii ni watu kutafuta uwezo wa kujisaidia zaidi ya kutegemea kusaidiwa hasa
katika mambo ya afya ya akili, hisia ,nk. Zaidi ya 40% ya tovuti za
masuala ya afya kutumiwa na watu hasa katika kutafuta kufahamu juu ya
tatizo la kupoaaza moyo na upweke (depression).
Huu ni wakati wa kila mmoja kujua jinsi ya kurekebisha maumivu yake na kuponya majeraha yake mwenyewe. Hii inawezekana.
Habari au taarifa nyingi za namna ya kujisaidia binafsi zimekuwa zikikosewa na kutafsiriwa tofauti mara nyingi. Hii ndio maana wengi wamekuwa hawatilii maanani na pia wengi kutopata matokeo halisi yanayotarajiwa. Safu ya gazeti hili leo inakwenda kukufungua na kukusaidia.
Yafuatayo
ni baadhi ya maeneo katika maisha yetu ya kila siku ambayo huleta
matatizo kwa kushindwa kuwa na ujuzi wa kujisaidia wenyewe.
1.Unapokuwa Katika Hasira Kali.
Kama vile yalivyomatundu katika kuta kubwa kwa ajili ya kupumulia hewa na kupunguza presha katika ukuta huo ili usije pata nyufa (ventilations) ndivyo hivyo mtu mwenyehasira kali
hutakiwa kujua jinsi ya kuyaruhusu mazingira aliyopo yaweze kumsaidia
kuipumulia nje ile hasira pasipo kuleta madhara kwake yeye na wale
wanaomzunguka ( venting anger )
Tumeona sana katika filamu au vitabu vya asili
ya nchi za magharibi wengi wakiwa katika hali hii hukumbatia au
kung’ata au kupiga ngumi mito ya kulalia (pillow) au wengine hutupa
ngumi katika mfuko wa mazoezi ya kupigana (punching bag) katika hali hii
hasira kali hupata pakupenyezea na kupoa. Watalaam
wameshauri kutumia nguvu zote kutupa ngumi au kupiga mito hii au
puching bag na kama ni mtu amekuudhi basi fikiria kuwa unauona uso wake
katika mto huo na uiachie hasira yako kimwili (kwa kupiga) na
kimaneno kwa kuongea yale yote yaliyo moyoni mwako. Watafiti wanasema
aina hii yaweza pia kuwa msaada kwa kupunguza msongo wa mawazao mbali na
hasira.
Tafiti za hivi karibuni zimeonyesha mtazamo wa tofauti kidogo katika hili. Dr Brad Bushman mwanasaikolojia wa
Iowa state university anasema watu wengi hufikiri kwa kufanya hivi
wanafanikiwa kupona hasira ila wale wachache ambao inashindikana
wanakuwa na hasira kali maradufu na kuchanganyikiwa.
Baadhi
ya tafiti zimeonyesha kuwa kukosewa kwa namna ya kuipunguza au kuitoa
hasira kumewasababishia wengi matatizo ya misuli ya kichwani na hivyo
kuhatarisha akili zao.
Nini Kifanyike Basi
i) Jaribu
kufanya chochote kile ambacho chaweza kikachukua nafasi ya hasira
moyoni, kila mtu anakitu anachokipenda, kifanye hicho sasa, kwa mfano;
kuangalia filamu, picha, kusoma au kusikiliza hadithi au kusikiliza
nyimbo unazozipenda, jihadhari kukaa karibu na yule aliyekukwaza mpaka
mmesuluhisha yaliyowasibu.
ii) Pata
muda wa kucheka na marafiki wengine, kama ni baba pata muda wakutoka na
watoto wako, hawa wananafasi kubwa ya kukuingia moyoni kwa haraka na
kusafisha hasira uliyonayo.
iii) Usikimbilie
sana kwenye mazoezi ya viuongo kwasababu utafiti wa Dr. Bushman
unaonyesha kuwa mazoezi ya viungo yananafasi kubwa ya kuiamsha hasira,
wengi waliotafitiwa walienda kupigana mara tu baada ya kumaliza mazoezi
ya viungo.
iv) Michezo
ya kijadi kama vile tai, chi, na yoga yaweza kuwa msaada wa kurekebisha
hisia na hali ya akili, ni vema ukafanya michezo hii kama unaujuzi nayo
na kama inaruhusiwa na imani yako, kwa sababu mingi iko zaidi katika
imani za dini za nchi za bara Asia.
v) Muendelezo
wa kufanya kazi au shughuli itakayochukua muda mrefu wa kufikiri na
kuifanya bize akili yako inaweza kupooza hasira pia.
2. Unapokuwa Umefadhaika, Umepooza, Unahuzuni na Kuvunjika Moyo
Tafuta sana kufikiria yale yaliyo mema na ya kukutia moyo. Peleka
moyo wako katika yale yanayokupa furaha zaidi kuliko katika yale
yanayovunja furaha yako. Funga milango yako ya akili, usiruhusu chochote
kisicho cha furaha kuingia ndani. Tumia ubongo wako kufikiri kuwa yote
yanawezekana (optimistic thinking).
Teka uwezo wa akili na fikra zako na uzielekeze kule tu unakopenda wewe,
usiruhusu kamwe watu au mazingira yakuletee picha inayokuumiza moyo
Tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi tunapokuwa katika huzuni na kuvunjika moyo kila kitu huonekana kinyume nasi. Nguvu ya ubongo nayo inashindwa kuyadidimiza yale yaliyo mabaya ili tusiyawaze. Na kila tunapojaribu kujitahidi wenyewe kuikataa hali hii mawazo na mitazamo ya kufeli na kushindwa hujaza fikra zetu. Mara unapojaribu kufikiri yale mema moto huwa mkali zaidi na kuona kuwa wewe ni wakushindwa zaidi.
Ufanye nini Basi?
i) Pata
muda zungumza na marafiki, watu wa dini (wachungaji, mapadri, shekhe,
washauri au yeyote anayeweza kukupa mitazamo ya tofauti na kukuwezesha
kuwaza mambo mengine.
ii) Nenda katika maeneo ambayo watu wanafurahi, kama vile sherehe, ufukweni, hotelini, super market au katika maduka makubwa, taratibu utaona roho na nafsi yako vinanyanyuka upya.
iii) Na
kama unajua kuwa kunakitu kitakuudhi na kuharibu furaha yako panga vitu
vingi vilivyo vyema na vyakukujenga utumie muda kuviwaza hivyo.
3. Unapojihisi Kupoteza Mwelekeo wa Maisha
Kumbuka
na uyafikirie tena na tena malengo yako, hii itakuwezesha kuyafanya
yawe kweli. Pata mawazo na picha ya wewe ukifanikiwa na sio ukishindwa,
iache picha hiyo ikae katika akili yako, itakusaidia kuyafanya matendo
yako yapiganie uhalisi wa kile kilichopo akilini mwako.
Kuwaza
tu kuwa unafanikiwa hakutoshi, hapa ninazungumza pia na wale wenye
imani zao kali za dini ambao hukesha wakiamini wanafanikiwa na
wamekwisha fanikiwa na wakati hakuna wanachokifanya, lazima ufanye
mabadiliko yakimtazamo lasivyo kifo kitakukuta hapo hapo ukiwaza
unafanikiwa wakati watu wanakuona wewe kama mfano mzuri wa walioshindwa
maisha. Lazima picha ulionayo ya kufanikiwa itiwenguvu na matendo(actions) ya kila siku katika kuifanya ndoto yako kuwa halisi “to make your dream come true”
Shelley Taylor, Daktari wa saikolojia wa chuo kikuu cha UCLA Marekani ameonyesha kuwa katika kufikiria tu kuwa unafanikiwa na
kuliwekea picha lengo lako katika akili bila matendo ina athari mbili;
Kwanza inalitenganisha lile lengo mbali na kile kinachohitajika kufanywa
ili lengo lifikiwe, na pili inakufanya ufurahie utamu wa kuwa mtu
aliyefanikiwa wakati bado kabisa hujafika popote, hali
hizi zinafifisha nguvu ya lengo lako (power of the goal) na kukufanya
kushindwa kujitahidi kufanya kazi na kukubali kupoteza (to take risks)
katika kukipata kile ambacho kiko katika ndoto zako za kila siku.
Nini kifanyike?
i) Pamoja
na kuwaza kila siku na kuwa na ndoto za mafanikio, pata wakati jiulize
ninini unaweza kufanya ili kufikia mafanikio hayo, na ukipata njia au
mbinu hizi anzia kuzifanyia mazoezi akilini kabla ya kuziweka katika
uhalisia.
ii) Kwa malengo ya muda mfupi waweza kupitia hatua zote ulizo zipanga ndani ya siku moja kabla ya kuanza kuzitendea kazi. Lakini kwa malengo makubwa na yamuda mrefu unaweza kupitia mipango yako tena na tena kadri unavyozidi kuendelea na mchakato mzima na uone kama kunahitajika marekebisho.
4. Unapokuwa na hali ya Kutojithamini na Kutojipenda (Low Self Esteem)
Jitambue ya kuwa wewe ni wathamani na ni mtubora zaidi. Hii
itakuwezesha kujithamini na kujipenda. Jifunze kuandika maneno ya
ushindi yanayoonyesha ujasiri na ukakamavu (affirmation) kwa mfano viko
vikaratasi vidogo vya kunatisha (stickers) katika kuta au katika magari
vinamaneno “every thing is possible” vikimaanisha kila kitu
kinawezekana. Nyingine zimeandikwa “I can do it’ (ninaweza), nakumbuka nimeona katika gari la rafiki yangu kikaratasi cheye
maneno ya dini “nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu” maneno haya
na mengine mengi yawe ya dini au yakutungwa au waweza kuandika mwenyewe
na kubandika katika ukuta wako, kioo cha kujitazama, katika mlango wa
friji yako, ndani ya gari lako, pembeni ya kitanda au bafuni. Kwa teknolojia ya sasa unaweza kuyarekodi maneno haya na yakasema katika redioyako mara kwa mara au kuyaandika katika compyuta yako yakawekwa kama “screen saver” ili mradi tu kila unapogeuka unayaona yanasema na wewe. Maneno haya yana nguvu ya kupenyeza ujumbe ndani ya fikra na moyo wako na kuruhusu mwili wako kudaka na kuyatendea kazi.
William
Swann, daktari wa chuoo kikuu cha Texas anasema mtazamo huu unaweza
kuwa mgumu kidogo na sio wote wanaweza kufanikiwa katika hili kwasababu
kubadili jinsi tunavyojihisi wenyewe ni kazi ngumu sana.
Hali
ya kujithamini na kujipenda inategemea mambo mawili; Kwanza hisia zetu
za jinsi gani tunavyojipenda, na pili hisia zetu za uwezo gani tulionao
katika kazi zetu na shuhuli nyingine zinazohitaji ujuzi na vipawa vyetu.
Katika hili matumizi ya maandishi yanayoonyesha
ushindi na kuweza (affirmations) yaweza kufanikiwa kwa baadhi ya watu
lakini pale yanaposhidwa kufanya kazi huweza kumuacha mtu akiwa ameumia
moyo zaidi.
Mara nyingi wale wenyemitazamo mibovu kuhusu wao wenyewe hawajiamini na hawaamini kama waweza kusema au kufanya kitu
bora hata siku moja kwa jinsi hii hata kama wakiandika vimaneno vingi
vilivyo vya kutia moyo bado hawatakuwa na imani maana wanachokijua wao
ni kwamba kamwe hakuna chema kitakachoweza kutoka kwao. “Nothing good shall ever come from them”
Nini kifanyike basi?
i) Njia pekee ya kubadilisha matunda ya vile tunavyojihisi au tunavyojithamini ni kubadili vile vinavyotuingia na kutengeneza ile hali ya jinsi tunavyojiona. Kwamfano; kama unajikuta unashindwa kujithamini au kujipenda sababu ya wale unaohusiana nao au
unaokuwa nao zaidi, basi badilisha,chagua watu wengine wakuhusiana nao,
labda hao watasema yaliyobora kuhusu wewe na kukutia moyo zaidi. Kama
uko katika ajira ambayo kila mtu anakuona wewe hujui na wewe
niwakushindwa tu, amua kuwataka wabadili mtazamo wao kwako au ikibidi ondoka pata kazi sehemu ambayo watu wanamtazamo mzuri kwako. Jaribu kufanya kazi yako vema zaidi ya ulivyoifanya kule kwa awali.
ii) Simama ujitetee mwenyewe usingoje kutetewa “stand for yourself”
hakikisha
unazungukwa na watu wanaokuona kuwa wewe ni wathamani, unayeweza, na ni
mtu mwema. Hakikisha wanalikiri hilo kwa vinywa vyao.Uwe mvumilivu na
wakati wote jitahidi kutimiza majukumu yako ili usiwavunje moyo wale
wanokuona wewe kuwa mtu mwema na wanayekuamini. Fahamu kuwa jinsi
tunavyojiona sisi wenyewe, na mtazamo tulionao kuhusu sisi wenyewe (self
esteem) ni mjumuisho wa jinsi tunavyohusiana na watu wanaotuzunguka kwa
muda tuishio hapa duniani na kwamwe hauwezi kubadilika kwa usiku mmoja.
5. Unatatizo la Mawasiliano Katika Mahusiano Uliyonayo:
Usikivu
makini (active listening) unaweza kukusaidia kuwasiliana vema na rafiki
yako au mpenzi wako. Katika usikivu makini tunamaanisha sio tu kusikia,
bali kuelewa kwa uhakika kile mwenzako anachojaribu kukisema. Hapa
ndipo tofauti kati ya neno “hearing” na neno “listening”
inapojidhihirisha na hata maneno kusikia na kusikiliza yanapoonyesha
tofauti. Katika mahusiano baina ya watu, marafiki, wapenzi, ni lazima kuwepo na kusikilizana “listening” na sio “kusikiana”
Mahusiano
mengi na hata ndoa nyingi zimekuwa na migogoro na hata mivunjiko maana
kumekuwa na kusikiana zaidi ya kusikilizana kamwe msisahau kuwa
tunayasikia magari, tunasikia ndege wa angani na ndege za abiria,
tunasikia upepo na miti na makelele mengine lakini tunawa sikiliza watu na yale wanayoyasema.
Tunasikiliza
kile tunachoelezwa kwa kukitathmini kama vile kilivyosemwa na
tunakirudia kwa maneno yetu wenyewe tukijaribu kifikiri kile mwenzetu
anachojaribu kutuambia. Katika
hili tunatambua yakwamba kusikiliza ni mchakato (process) wakati sio
hivyo katika kusikia. Baadhi ya wachunguzi wamegundua kwamba usikivu
makini au masikilizano, yanawasaidia zaidi wale walioko katika mahusiano
mazuri, lakini maranyingi mchakato mzima wa kusikilizana hukwama hasa
pale wapenzi wanapokuwa katika ugomvi au mahojiano makali, hapa
kusikilizana huwa ni ndoto.
Zingatia haya!
Walioko katika mahusiano (wanandoa) wajaribu kupeleka jitihada zao zote katika mambo matatu muhimu
i) wanawake
wajitahidi kuwasilisha hoja na madai yao katika hali ya upole na
upendo. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume wengi wamekuwa tayari kusikiliza
toka kwa wanawake pale ambapo wanaongeleshwa kwa utulivu na
unyenyekevu.
ii) Wanaume wanahitaji kuwasikiliza wenza wao kiufasaha na kuzingatia juu ya hisia na mawazo yao.
iii) Pande zote mbili yaani wanaume na wanawake jitahidini kwa kila hali kuutuliza utu wa kiume na kuutiisha. Kiasili
wanaume wanatabia ya kuhemka nakuwaka hisia zao za hasira haraka hasa
wanapogadhibishwa, na kwa hali hii hujitahidi kujitoa kwenye tatizo
haraka ili waziponye nafsi zao hatakama ufumbuzi wa tatizo haujapatikana
na hii hufanya matatizo mengi katika mahusiano kuachwa bila suluhisho
“unsolved Conflicts” na hali hii pia huwaacha wanawake katika hasira na
maumivu makali.
Jitahidini
kuhakikisha hamfikii katika hali hii kwa kurushiana utani kidogo au
mwanamke kumkumbatia mwanaume angalau kupunguza gadhabu yake na mara
mtajikuta mnaishia pazuri.
No comments:
Post a Comment
YOUR WORMY WELCOME TO SAY ANYTHING TO ME IN MY WEBSITE