Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.Kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
Mazingatio.
- 1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
- 2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
I.Tumia
programu za uhakika
Je umewahi kujiuliza kwanini
natumia programu hii badala ya ile? Ukuaji wa teknolojia umesababisha kila mtu
kuja na programu yake,kuna zile za bire,za kugawana na hata zile za bei
chee.Sasa sitaki kusema kuwa programu za bei ya juu ndio bora au zile za bei ya
chini ni za kukimbiwa kama ukoma,ila wewe kama mtumiaji unatakiwa kufanya
kautafiti kadogo kabla ya kuamua kutumia programu fulani. Siku hizi kuna google
ambayo inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya utafiti na kuangalia maoni
ya watumiaji juu ya programu husika.
Kwa kufanya hivi itakusaidia
unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri
binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na
kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi
wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na
Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na kuleta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha
wengi. Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
II.Hakikisha
unajua nini unachokifanya
Wengi wetu tumekuwa wahanga
kutokana na kukubali kiholela au kufanya mambo tusiyoyajua.Labda nikupe mfano
mmoja wa mtu wangu wa karibu ambaye aliwahi kuvamiwa na na hizi programu za
matangazo(Adware).Yeye alikuwa alifungua tovuti moja mara akaona ujumbe unasema
kompyuta yako ipo hatarini hivyo bonyeza hapa ili kutatua.Bila kujua
anachokifanya akabofya na kujikuta ameshaingiza madudu kibao.
Hivyo kuwa makini kila
unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
Hayo ni mabo machache ambayo
unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye
kinga bora.
No comments:
Post a Comment
YOUR WORMY WELCOME TO SAY ANYTHING TO ME IN MY WEBSITE