MUOGOPE MUNGU AWEZAYE KULEFUSHA SIKU ZAKO MWABUDU YEYE TU

WELCOME

WELCOME TO MY WEBSITE AND LETS SHARE WHAT YOU HAVE BY CLICKING COMMENTS TO ANY INTERESTED ARTICLES AND LEAVE YOUR COMMENTS THERE STAY BLESSED

Saturday, January 19, 2013

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Marufu Tanzania

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Maarufu Tanzania

Mungu ameibariki Tanzania Kwa Kila aina ya Baraka za Mwilini na rohoni. Leo na wiki chache zijazo nitakujuza Watumishi 25 ambao ukiwataja kwenye mikoa zaidi ya Kumi hapa Tanzania yamikini wameshasikika na unaweza pata comments toka kwa waumini wao. Kuna Makanisa ambayo pengine yamesikika zaidi kuliko kuliko majina ya watumishi hao ama kuna watumishi wamesikika zaidi kuliko hata Makanisa wanayochunga.

Kuna Watumishi ambao wamekuwa maarufu sababu ya huduma zao kwa Ujumla, Sababu utajiri wao, sababu za huduma zao kwa wanafunzi ama kwa program zao za mahali pamoja.

lengo la Makala haya si kutafuta nani yuko Juu zaidi ya mwingine ila kutoa taarifa kwa umma na kuwatia moyo watumishi hawa kuwa kazi yao imevuka mipaka ya mikoa na nchi.

Tahadhari
Yawezekana vigezo vyako sio vugezo vyangu katika kuwasilisha.

Apostle Maboya(Ni kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania

Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini


Mwalimu Christopher Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya New Life Crusade/ New Life in Christ.



Mchungaji Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.



Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.




Mtume Veron Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.


Askofu Moses Kulola wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila kona ya Tanzania

Nabii GeorDavie wa GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.

Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.


Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM) na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.

ni hao kwa leo tutaendelea kukujuza zaidi endelea kufuatilia

Sunday, January 6, 2013

UNAWEZA KUPUNGUZA UNENE KWA KULA VYAKULA VIFUATAVYO



NI ndoto ya WATU WENGI wengi wanene kupunguza unene, lakini wengi wao hawajui wafanye nini. Zipo njia nyingi za kumfanya mtu apunguze unene, miongoni mwa njia hizo ni pamoja na vyakula, kujua aina ya vyakula unavyotakiwa kula na kuvila kama inavyoelekezwa.
Tikitimaji.
Vifuatavyo ni vyakula, mboga na matunda ambayo yakiliwa kwa mpangilio mzuri huondoa mafuta ya ziada mwilini na hivyo kupunguza unene wa ziada. Vyakula hivi vina sifa ya kuchoma yenyewe mafuta kabla ya kuhifadhiwa mwilini:


Machungwa.
MATUNDA
Matunda ni miongoni mwa vyakula vinavyoyeyusha mafuta mwilini, idadi kubwa ya mtunda huwa na kiwango kidogo cha kalori (calories) lakini yana kiasi kingi cha kamba lishe (fibre).
Matunda yenye kamba lishe nyingi huyeyusha mafuta mwilini haraka kwa kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na humuongezea mtu nishati ya mwili. Kwa sababu hii, unaweza kuchanganya ulaji wa matunda na vyakula vyenye mafuta bila kuongezeka unene. Matunda kama epo, machungwa, zabibu, mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiasi kingi cha kamba lishe.

Mapera.
Vilevile, tikitimaji lina faida kubwa mwilini, kwani lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini (toxins) ambayo huingia mwilini kwa njia ya chakula na hewa tunayoivuta kutokana na hali halisi ya maisha ilivyo. Pia tikitimaji linapoliwa huondoa maji ya ziada mwilini, pendelea kula tikitimaji kila wakati unaposikia tumbo kujaa au kuchafuka.
KABEJI
MBOGA ZA MAJANI
Mboga nyingi za majani huwa na kiasi fulani cha kamba lishe, na kamba lishe iko katika makundi mawili, ya kwanza ikiwa ni ile inayoyeyuka mapema na ile isiyoyeyuka mapema, mbogamboga zinazochukua muda kuyeyuka tumboni lakini zinasaidia sana usagaji wa chakula haraka ni pamoja na mchicha, spinachi, kabeji, maharage ya kijani na nyingine jamii ya majani kibichi.

PROTINI
Idadi kubwa ya vyakula vinavyoyeyusha mafuta haraka mwilini katika jamii ya vyakula vya protini ni vyakula vya baharini. Ingawa samaki huhitaji nishati nyingi kuyeyushwa mwilini, lakini ni miongoni mwa vyakula vinavyosaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini kwa haraka zaidi. Ili kupata matokeo mazuri na ya haraka, pendelea kula vyakula vya baharini sambamba na mboga za majani kama vile kabichi au saladi ya mbogamboga mchanganyiko.
Vilevile kuna aina nyingine ya vyakula ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuyeyusha mafuta ya ziada mwilini kama vile vyakula vitokanavyo na maziwa, ngano isiyokobolewa, wali, ambavyo wakati wa kutayarisha unatakiwa kuhakikisha vinakuwa na kiwango kidogo cha mafuta asilia bila kuongezewa ya ziada. Ukizingatia ulaji wa vyakula vilivyoanishwa hapo juu kwa wingi, bila shaka utapungua mwili au hutaongezeka mwili zaidi ya ulivyo sasa.

MBEGU ZA MABOGA ZINA UWEZO WA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 10 HATARI



ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
UGONJWA WA MOYO
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia (magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha  usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.
KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
MAFUTA YA OMEGA -3
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.
KIBOFU CHA MKOJO
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.
KINGA DHIDI YA SARATANI
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
UGONJWA WA KISUKARI
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.
AFYA YA MOYO NA MAINI
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.
DAWA YA USINGIZI
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri na tulivu.
DAWA YA UVIMBE
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu.

KANUNI BORA ZA USALAMA WA KOMPUTA




Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.Kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
Mazingatio.
  • 1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
  • 2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
I.Tumia programu za uhakika
 Je umewahi kujiuliza kwanini natumia programu hii badala ya ile? Ukuaji wa teknolojia umesababisha kila mtu kuja na programu yake,kuna zile za bire,za kugawana na hata zile za bei chee.Sasa sitaki kusema kuwa programu za bei ya juu ndio bora au zile za bei ya chini ni za kukimbiwa kama ukoma,ila wewe kama mtumiaji unatakiwa kufanya kautafiti kadogo kabla ya kuamua kutumia programu fulani. Siku hizi kuna google ambayo inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya utafiti na kuangalia maoni ya watumiaji juu ya programu husika.
 Kwa kufanya hivi itakusaidia unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na kuleta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha wengi. Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
II.Hakikisha unajua nini unachokifanya
 Wengi wetu tumekuwa wahanga kutokana na kukubali kiholela au kufanya mambo tusiyoyajua.Labda nikupe mfano mmoja wa mtu wangu wa karibu ambaye aliwahi kuvamiwa na na hizi programu za matangazo(Adware).Yeye alikuwa alifungua tovuti moja mara akaona ujumbe unasema kompyuta yako ipo hatarini hivyo bonyeza hapa ili kutatua.Bila kujua anachokifanya akabofya na kujikuta ameshaingiza madudu kibao.
 Hivyo kuwa makini kila unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
Hayo ni mabo machache ambayo unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye kinga bora.

Thursday, September 6, 2012

LISHE NA MATUNDA NA FAIDA ZAKE

UNAZIJUA FAIDA HIZI 9 ZA CHUNGWA?
 NI msimu mwingine wa machungwa, yamejaa tele kila kona. Shilingi 100 tu unapata chungwa. Lakini siyo ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala hata chungwa moja, wala suala la matunda halipo kabisa katika orodha ya milo yao!
 Inawezekana pia hata kwa wale wanaokula, japo kidogo, hula kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini. Katika makala ya leo nitakujuza faida 9 unazoweza kuzipata unapokula chungwa, ambalo limesheheni virutubisho kibao.
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila linakidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.
1.UKOSEFU WA CHOO
Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

4. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

5. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

6. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

7.  VIDONDA VYA TUMBO
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.

8. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadri uwezavyo ili ujiepushe na mafua kwa sasa.

9. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohoo, kifua kikuu, nimonia na kisukari.

Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.

Saturday, April 7, 2012

MUACHE MUNGU AITWE MUNGU HAWA WAMEMTUMIKIA MUNGU NA WENGINE WANAANZA KUMTUMIKIA MUNGU

HAPO JUU NI WATUMISHI WA MUNGU WAKISIMIKWA KATIKA HUDUMA YAO YA KUMTUMIA MUNGU KAMA VIONGOZI_ CCT KATIKA CHUO KIKUU CHA RUAHA IRINGA 
WAKATI WENGINE WAKIAGWA KATIKA HUDUMA HIYO PIA KWA NJIA YA MSHUMAA KAMA ISHARA YA KUANGAZA KATIKA HUDUMA HII MUNGU AWABARIKI WOTE WALIOHUSIKA .

Thursday, December 8, 2011

TAMANI KUMTANGAZA YESU PAMOJA NA MTUMISHI WA MUNGU (Mwl MTAKA)

Hapo juu Mwl Mtaka akifundisha katika chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) Kabla ya yeye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCT RUCO
HAPO JUU MWALIMU MTAKA AKIKABIZIWA MSHUMAA KWA ISHARA YA KUANGAZA KATIKA UONGOZI WAKE KWANI AMECHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCT (chuo kikuu cha Ruaha)  RUCO NA HUYO MBELE YAKE NDIYE ALIYEMKABIZI BAADA YA MDA WAKE KUISHA.

Tuesday, September 27, 2011

tumpende Mungu

MUNGU AKUBARIKI SANA WAPENDWA MNAOITAKIA  MEMA NA KUIOMBEA  BLOG HII IWABARIKI WATU WOTE WA RIKA MBALIMBALI BILA KUBAGUA MAANA NATAMANI SANA WATU WENGI WAMJUE MUNGU KUPITIA BLOG HII NAOMBA UFANYIKE KUWA BARAKA KWA KUWATAARIFU WATU WENGINE ILI WASONGE MBELE KIROHO ILI WOTE TUWEZE KUFIKA MBINGUNI AMINI MUNGU ANAWEZA YOTE KATIKA MAISHA YETU.

Tujifunze biblia/Bible Teaching